KAMPUNI ya AGAPE
televisheni imezindua na kuanza
kuuza kisimbusi chake cha aina ya TING mkoani Rukwa ili kutoa fursa kwa wakazi
wa mkoa huo kuanza kutumia teknolojia ya digitali ambapo wataweza kuona channel
nyingi tofauti na kutumia teknolojia ya Analojia ambayo haitoi fursa ya kupata chaneli nyingi
kama ilivyo kwenye Digitali.
Akizindua kisimbusi
hicho kwa niaba ya mkuu wa mkoa
huo ,makamu mwenyekiti wa
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
Emmanuel Malisawa alisema kuwa hii ni fursa kwa wakazi wa mkoa
huo kuingia katika mfumo wa digital mapema zaidi kuliko kusubiri mpaka serikali
itakapo zima mitambo ya Analojia ndipo waanze kutumia visimbusi vitakavyo
wawezesha kupata matangazo ya televisheni.
Alisema kuwa
mabadiliko hayo ya kiteknolojia ni fursa nzuri kwa wakazi wa mkoa huo
ambao ulikuwa haupati vyombo vya habari vingi katika mfumo wa analojia lakini
kwa mfumo huu mpya wakazi wake watakuwa na uamuzi wa kuchagua kuangalia
televisheni wanayotaka.
Naibu meya alisema kuwa kutokana na madiliko hayo wakazi wa
Rukwa wanafursa ya kujua mambo mengi ikiwemo na masuala ya kibiashara ambapo
kupitia ongezeko la vyombo vya habari wataweza pia kujua bei ya vitu mbalimbali
ikiwemo soko la zao la mahindi ambalo imekuwa ni tatizo kwa wakulima waliopo
mkoani humo.
Kwaupande wake mkurugenzi wa
Kampuni ya Agape Televisheni Vennon
Fernandos wanaomiliki kisimbusi cha TING
alisema kuwa wameamua kuja mkoani Rukwa kwa nia mbili kwanza ikiwa ni
kutoa fursa kwa wakazi wa mkoa huo kuingia katika mfumo wa digitali mapema
zaidi ambapo watapata nafasi ya kusikia na kujifunza mambo ya watu wengine
sambamba na wao kutangaza yakwao.
Alisema kuwa sababu nyingine ni kuhubiri neno la mungu
kupitia chaneli za kidini zinazopatika katika kisimbusi hicho ambapo kinaongeza
wigo wa kusikia neno la Mungu hata ukiwa nyumbani kwako injili itakufikia hapo
ulipo.
No comments:
Post a Comment