Na Gurian Adolf
Kalambo
WAVUVI wa samaki katika ziwa Tanganyika wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameishukuru serikali ya Zambia kwa kuondoa marufuku ya biashara ya samaki katika nchi hiyo ambayo ilikuwa imewekwa kwa takribani wiki mbili kutokata na kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu nchini humo.
Shukrani
hizo wamezitoa jana wakati wakizungumza na mwandishi wa habari wa gazeti
hili ambapo walisema kuwa marufuku hiyo ilikuwa imewaathiri kiuchumi
kutokana na kuwa soko kubwa la samaki wanaovuliwa katika ziwa Tanganyika
wilayani Kalambo mkoani Rukwa nchini Tanzania ilikuwa ikitegemea soko
katika nchi hiyo jirani.Kalambo
WAVUVI wa samaki katika ziwa Tanganyika wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameishukuru serikali ya Zambia kwa kuondoa marufuku ya biashara ya samaki katika nchi hiyo ambayo ilikuwa imewekwa kwa takribani wiki mbili kutokata na kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu nchini humo.
Sichone alisema kuwa
katika nchi hiyo kuna makampuni 12 ambayo yamekuwa yakinunua samaki tani
1,200 kila siku ambapo kilo moja wavuvi wamekuwa wakiuza kwa
shilingi 5,000 za kitanzania lakini katika kipindi ambacho nchi hiyo
ilipiga marufuki ya biashara ya samaki soko lilishuka ambapo walikuwa
wakiuza kilo moja kwa shilingi 1,500 na kulikuwa kuna kampuni moja tu ya
Premji iliyopo Kasanga ambayo ilikuwa inauwezo wa kununua tani nane za
samaki.
Naye Michael Sichilima mvuvi wa kijiji cha
Kapele katika mwambao wa ziwa Tanganyika wilayani kalambo alisema kuwa
kitendo ilichokifanya serikali ya Zambia ni chakupongezwa kwani kimetoa
fursa ya biashara si tu kwa wavuvi wa nchini humo lakini pia wavuvi
kutoka nchi jirani watanufaika.
Aliwasihi wavuvi
kutoka mkoani wilayani humo kuheshimu sheria za nchi hiyo pindi
wanapokwenda kufanya biashara ya samaki ili wasije kugeuka kero na
kusababisha kuharibu uhusiano wa kibiashara na u dugu baina ya wanachi
wa nchi hizo mbili kwakua mahusiano yao ni ya kihistoria na yanafaa
kulindwa kwa maslahi ya waafrika wote.
Mwisho
No comments:
Post a Comment