Na Gurian Adolf
Nkasi
WAZIRI wa maji na umwagiliaji mhandisi Isack Kamwelwe
ameagiza kuundwa timu maalumu ambayo
itakuwa na kazi ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa mkoani Rukwa kutokana
na kuwa na mapangufu mengi ya kiufundi ambayo aliyabaini wakati akiwa anakua
miradi hiyo.
Agizo hilo alilitoa jana katika Kata ya Kabwe wilayani Nkasi
katika mkutano wa hadhara baada ya kubaini mfumo wa umeme wa jua unaotumika
katika mashine ya kusukuma maji katika tenki kuwa hazina kiwango ambapo alidai
kuwa haziwezi kudumu kwa muda mrefu.
Alisema kuwa yeye binafsi akiwa ni waziri mwenye dhamana
hajaridhishwa na kasoro nyingi alizoziona baada ya kukagua mradi wa maji wa
Kabwe ambao umejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.1 lakini ueonekana kuwa
na changamoto hata kabla ya kuanza kutumika.
Waziri Kamwelwe alisema kuwa ameona mfumo huo wa umeme
uliotengenezwa na kampuni ya A and O Consultant yenye makazi yake jinini Dar es
salaam kuwa vifaa vilivyotumika havina ubora unaotakiwa hivyo ameagiza wizara
yake iunde timu ya wataalamu watakao kagua miradi yote ya maji mkoani humo.
Alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya Nkasi inamiradi ya
maji nane yenye thamani ya shilingi bilioni 19 lakini miradi mingi inaonekana
inahitilafu za kiufundi hivyo haina budi kukaguliwa ili kujiridhisha kwani
serikali haipo tayari kuona fedha za walipa kodi zinachezewa hovyo.
‘’naagiza lazima iundwe timu ya wataalamu kutoka wizarani
wafike kukagua miradi yote ya maji katika mkoa wa Rukwa,kwani imekuwa
ikilalamikiwa sana, serikali ya awamu ya tano haitavumilia kuona fedha za
walipa kodi zinatumiwa vibaya na watu wachache kwa manufaa yao’’ alisema.
Awali akimkaribisha waziri huyo afisa tawala wa wilaya ya
Nkasi Festo Chonya alisema kuwa miradi ya maji inayotekelezwa wilayani humo
imekuwa na changamoto nyingi ambapo inaonekana baadhi ya watekelezaji wamekuwa
wakihujumu kwa makusudi.
Alisema kuwa miradi hiyo iliyotekelezwa imetumia fedha
nyingi lakini kunahofu kuwa haitadumu kwa muda mrefu kutokana na vifaa vilivyo
tumika kutokuwa imara kwani baadhi vimeanza kuharibika hata kabla ya miradi
kuzinduliwa.
Naye mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini Ally Kessy aliwashauri
wananchi kuacha tabia ya kujisaidia ziwani kwani wamekuwa wakisababisha
miripuko ya magonjwa kama kipindupindua mara kwamekua wakitumia maji hayo ya
ziwani kwa kunywa bila kuchemsha.
Alisema kuwa ziwa hilo maji yake bado ni masafi kwani
hayachafuliwa na kemikali mbalimbali changamoto iliyopo ni wananchi kujisaidia
ziwani kutokana na kutochimba vyoo kitendo ambacho ni hatari kwani miradi ya
maji inachukua maji hayo ya ziwa kwenye mabomba na kuwapelekea wananchi
kwaajili ya matumizi yao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment