Na Israel Mwaisaka
Nkasi
WANAFUNZI wawili wilayani Nkasi Mkoani Rukwa wamenusurika kifo baada ya kugongwa na kujeruhiwa na gari la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika kijiji cha
Paramawe wilayani Nkasi mkoani humo.
Akizungumzia tukio hilo lililotokea jana majira ya saa 8;15 mchana
katika kijiji cha Paramawe Kamanda wa Polisi mkoa
wa Rukwa George Kyando aliwataja majeruhi hao kuwa ni
Trivol Julius (12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya
Msingi Paramawe na Isack Lusembo (17) ambaye ni Mwanafunzi wa
Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mtenga .
Alisema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa
dereva ambaye jina lake limehifadhiwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini walieleza kuwa Isack
ambaye ni mwanafunzi wa Kidoto cha Nne kabla ya ajili hiyo alikuwa amembeba
Trivol kwenye baskeli aliyokuwa akiendesha katika baraba ku itokayo
Tunduma mkoani Mbeya kwenda Mpanda mkoani Katavi katika eneo la kijiji cha
Paramawe.
Naye mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda ambaye jana usiku aliwatembea
majeruhi hao ambao wamelazwa katika hospitali Teule ya Wilaya (DDH)
iliyopo mjini Namanyere kwa matibabu alisema kuwa hali zao ni mbaya
kwamba wanatarajiwa kuhamishiwa katika Hospitaliya rufaa ya mkoa wa
Rukwa iliyopo mjini Sumbawanga kwaajili ya matibabu zaidi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment