Thursday, 1 March 2018

Polisi watakiwa kuwa waadilifu

Na Walter Mguluchuma
Katavi
WATENDAJI wa jeshi la polisi mkoani Katavi  wametakiwa kufanya  kazi  zao kwa  kuzingatia maadili na uzalendo ili   waendelee kuaminiwa na  kujijengea  heshima kwa jamii.
Kamanda wa polisi mkoani humo Damas Nyanda aliyasema hayo jana katika   kantini ya  Polisi wakati wa hafla  ya  makabidhiano ya bati  bandro  40 zilizotolewa  na  wadau pamoja  na askari polisi kwaajiri ya  ujenzi  wa ukumbi wa kisasa utakao tumika kwaajili ya mikutano  na  sherehe.
Alisema kuwa ili  polisi  aweze   kujijengea  heshima  kwa jamii ni  lazima  wafanye  kazi  kwa  kuzingatia   maadili na  wawe  wazalendo  na hali itakayo wajengea heshima na imani.
Kamanda Nyanda alisema kuwa kutokana na polisi hao kutenda kazi kwa uweledi wadau hao wamewachangia michango  mbalimbali ambayo imefikia kiasi cha shilingi milioni 31,221,000.00  ambapo kati ya fedha  hizo  Shilingi  milioni   12,129,000  zimechangwa  na  askari  polisi na shilingi  milioni 19,092,000 zimechangwa na wadau wengine wa maendeleo.
 Aidha kamanda huyo wa polisi aliwashuru  wadau  wote  waliochangia na  kuwaomba  waendelee  na  moyo huo  na  usiwe  kwa   polisi  pekee  bali wafanye hivyo na  kwenye  taasisi  nyingine  pia   ambazo zinahitaji  misaada ya  michango ya maendeleo.
Naye mkuu  wa  wilaya  ya  Mpanda   Lilian  Matinga   alisema  kuwa  mkoa  wa  Katavi  unao wadau  wengi wa  maendeleo na  wamekuwa  wakichangia  kwenye  maswala  mbalimbali  ya maendeleo  kwenye  jamii  kama  vile   elimu   afya  na   maji.
Kwa upande wake mbunge  wa  Jimbo  la Mpanda  mjini   Sebastiani  Kapufi  alisema yeye kama   Mbunge  hataacha   kuwazungumzia  askari  polisi  ndani na  nje ya bunge  juu  ya  changamoto  walizonazo askari  hasa suala la nyumba  za kuishi.
Alisema askari  polisi  wanafanya  kazi  kubwa ya  kulinda  usalama wa  raia  na  mali zao  na  jitihada   hizo zinaonekana katika  mkoa  wa   Katavi  kwani  wameweza kupunguza   matukio ya  uharifu na  ujambazi  yaliyokuwepo  miaka ya  nyuma  katika   mkoa  huo   hali  ilyokuwa ikiwalazimisha baadhi ya  wafanyabiashara  kuhama  nyumba  zao    nyakati za  usiku  kwa  kuhofia  kuuawa.
Katika hafla hiyo msimamizi  wa  mradi  huo  mratibu wa  polisi Kway   Ngoroma   alisema kuwa fedha   hizo   walizopata  watahakikisha  wanazitumia vizuri na  kwa  malengo yaliokusudiwa  na  singinevyo.
Alisema mbali ya   mradi  huo  wa  ujenzi wa  ukumbi wa   mikutano pia kunasuala la ujenzi wa  zahanati ya polisi ambao unaendelea  ambayo   ikikamilika   itasaidia   askari polisi  kupatiwa  matibabu na  jamii   ya wakazi  wa  manispaa ya  Mpanda kwa ujumla.
Mwisho

No comments:

Post a Comment