Na Gurian Adolf
Nkasi
JUMLA
ya walimu 16 wamefukuzwa kazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa kwa kipindi
cha miaka mitatu na wengine 11 wamepewa onyo kali baada ya kubainika
wametenda makosa mbalimbali.
Katibu wa tume ya utumishi wa walimu TSC wilayani
humo Richard Katyega aliyasema hayo jana mbele ya kamishina wa tume ya
Utumishi wa walimu Taifa, Samwel Koroso ambapo alisema kuwa katika
kipindi hicho walipokea mashauri 23 na kupelekea walimu 16 kufukuzwa
kazi,11 kupewa onyo kali na wengine 5 waliondolewa kazini baada ya
kubainika kuwa na vyeti bandia.
Alisema
kuwa katika mwaka wa fedha wa 2016, 2017 na 18 tume hiyo imeweza
kusikiliza mashauri hayo na kuyatolea maamuzi ambapo ilifikia maamuzi
hayo baada ya kusikiliza mashauri hayo na pasipo kumuonea mwalimu hata
mmoja na kutenda haki kwa mujibu wa sheria.
Katyega
alisema kuwa tume hiyo sambamba na kuchukua maamuzi hayo pia imekua
ikiwahamasisha walimu kufuata maadili ya ualimu kwa uhakika ili wasiweze
kukumbana na adhabu mbalimbali ikiwemo kufukuzwa kazi kwa mujibu wa
sheria.
Kwa
upande wake kamishna wa tume ya TSC Samwel Koroso alionyesha
kusikitishwa na vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa waalimu hali
inaoyopelekea kufukuzwa kazi na kuwa wao kama tume ya maadili kwa
walimu wataendelea kuwachukulia hatua Walimu wote ambao watakwenda
kinyume na maadili ya ualimu
Aliwataka
walimu kwenda sambamba na misingi ya sheria ya utumishi kwa walimu kama
inavyowataka na kuongeza kuwa walimu wilayani humo hawanabudi kuzipitia
sheria za utumishi wa walimu ili waweze kuishi kwa kufuata sheria hizo
zinavyo agiza.
Maofisa
kutoka ofisi ya ya kamishina wa tume hiyo nao waliweza kutoa mada
mbalimbali zilizolenga kuwapatia elimu Walimu na kuwakumbusha sheria za
utumishi wa walimu,huku walimu kwa upande wao walipata fursa ya kueleza
changamoto zinazo wakabili na zilipatiwa majibu kutokana na maswali
waliyokuwa nayo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment