Wednesday, 7 March 2018

TRA kuwabana wasiodai risiti

Na Gurian Adolf
Sumbawanga

WATEJA  wa bidhaa mkoani Rukwa wameonywa tabia ya kutodai risiti kwani wanaweza kujikuta wakifungwa jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 4.5
Akizungumza jana mjini Sumbawanga katika maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi meneja wa mamlaka ya mapato TRA mkoani humo Fredrick Kanyilili alisema kuwa wateja hao wa bidhaa mbalimbali wanapaswa kutii sheria ya mwaka 2015 kifungu cha 86 ambayo inatoa adhabu hiyo.
Alisema kuwa ni kosa la kisheria kwa mteja kufanya manunuzi bila kudai risiti lakini wateja wengi wamekuwa hawazingatii hilo kitendo ambacho ni hatari kwao kwani wanaweza kwenda jela.
Meneja huyo alisema kwa kwawaida malaka hiyo imekuwa ikitoa adhabu kwa wafanyabiashara kitendo kinachosababisha wateja wao kubweteka na kutotai risiti kanakwamba wao hawavunji sheria.
''sasa malaka ya mapato inaanza kula sahani moja na wanunuaji wa bidhaa nao wamekuwa ni kikwazo katika matumizi ya mashine za EFDs kwani hawana tabia ya kudai risiti,nadhani sasa ni zamu yao nao waonje joto la jiwe alisema.

Naye meneja msaidizi mkaguzi wa TRA mkoani humo  Amina Shamdas alisema kwa upande wa wafanyabiashara wao wameanya kuwa na mwitikio mzuri katika matumizi ya mashine za EFDs ambapo mpaka sasa mkoa mzima una wafanyabiashara 430 wanatumia mashine hizo.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo lakini wapo wachache ambao bado ni wakaidi na  jitihada zinaendelea kukabiliana nao kwani lengo la mamlaka hiyo ni kuona wafanyabiashara wote wanatumia mashine za EFDs.

Shamdas alisema kuwa upande wa vituo vya kuuzia mafuta mkoani humo wao wametii maelekezo ya kutumia mashine za EFDPs na mpaka sasa hakuna kituo ambacho kimekiuka agizo hilo.
Mwisho

No comments:

Post a Comment