Na Gurian Adolf
Sumbawanga
Wakazi wa mkoani Rukwa wametakiwa kuacha tabia ya kutelekeza wagonjwa wao hospitalini kwa kisingizio cha kukwepa gharama za matibabu kwani kufanya hivyo kunazipa mzigo mkubwa hospitali wa kuwahudumia wagonjwa hao.
Sumbawanga
Wakazi wa mkoani Rukwa wametakiwa kuacha tabia ya kutelekeza wagonjwa wao hospitalini kwa kisingizio cha kukwepa gharama za matibabu kwani kufanya hivyo kunazipa mzigo mkubwa hospitali wa kuwahudumia wagonjwa hao.
Katibu
wa afya wa hospitali ya Kristu Mfalme, Sista Yasinta Rugabagi alisema
hayo jana wakati akitoa taarifa ya hospitali hiyo wakati wa maadhimisho
ya kikanisa ya siku ya wauguzi duniani yaliyoambatana na ibada ya
kuwaombea wagonjwa waliolazwa hospitalini yaliyofanyika Katika hospitali
hiyo iliyopo mjini hapa.
Sista
Yasinta alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wananchi
kutelekeza wagonjwa wao waliougua kwa muda mrefu na kulazwa Katika
hospitali hiyo, kitu ambacho kinailazimu hospitali kuwahudumia kila kitu
kuanzia gharama za matibabu yao na chakula kwa siku zote wanazokuwa
wakipata matibabu kwenye hospitali hiyo.
Alisema
hali hiyo imekuwa ikisababisha hospitali kuelemewa na mzigo mkubwa wa
kuwahudumia wagonjwa wao kwa kuwa inakabiliwa na changamoto ya fedha
hivyo ifike wakati jamii ibadilike na kuachana tabia hiyo kwani
kuendelea kufanya hivyo ni kutokuwa na upendo kwa wagonjwa hao.
Pia
alitaka jamii kujenga utamaduni kutembelea wagonjwa na kutoka misaada
mbalimbali kwa wagonjwa si tu wanaolazwa Katika hospitali hiyo lakini na
maeneo mengine kwa kuwa wagonjwa wanahitaji kufarijiwa nyakati zote.
Awali,
meneja wa mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Simon Mbaga alizitaka taasisi
zilizo chini ya Kanisa Katoliki jimbo la Sumbawanga kujiunga na mfuko wa
Bima ya afya ili watumishi wao wawe na uhakika wa kupata matibabu pindi
wanapougua maradhi mbalimbali.
Alisema
kuwa baadhi ya watumishi wa taasisi hizo wamekuwa wakitumia gharama
kubwa kupata matibabu kutokana na kutojiunga na bima ya afya hivyo wana
fursa ya kujiunga na mfuko huo kupitia mpango wa uanzishwaji wa vikundi.
Aisha,
Kaimu mganga mkuu wa mkoa, Emmanuel Mtika aliwataka wananchi kujenga
utamaduni wa kijitolea damu ikiwa ni njia mojawapo ya kuwasaidia
wagonjwa wenye mahitaji ya kuongezewa damu ili kuokoa maisha yao.
Alisema
mahitaji ya damu bado ni makubwa Katika mkoa wa Rukwa, ambapo kwa mwezi
huitajika lita 200 hadi 300 ambazo husaidia sana kuokoa maisha ya
wakinamama wajawazito pindi wanapopungukiwa na damu baada ya kufanyiwa
upasuaji.
Mwisho
No comments:
Post a Comment