Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WAJUMBE waliochaguliwa katika nafasi ya utekelezaji ya umoja
wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT
mkoa wa Rukwa wametakiwa kuachana na dhana kuwa katika nafasi hiyo
watafanikiwa kiuchumi kwani kazi yao kubwa wapon kwaajili ya kujitolea kwa
maslahi ya chama.
Mwenyekiti wa umoja huo Merry Kalula aliyasema hayo jana wakati akifunga
baraza maalumu la UWT mkoa lililoketi katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya
Sumbawanga kwaajili ya kuwachagua wajumbe wanaounda kamati ya utekelezaji wa
umoja huo.
Alisema kuwa iwapo kuna mjumbe amegombea nafasi ya ujumbe wa
utekelezaji kwa nia ya kutafuta mashahi ni vizuri akajiuzuru ili nafasi yake ikajazwa
na mjumbe mwingine kwani kazi inayofanywa ni kujitolewa na wala si kutafuta
kipato.
Kalula alisema kuwa sehemu kubwa ya chama hicho
wanajitolea,hakuna maslahi yoyote ya kiuchumi wanayoyapata na wanawajibika
kukipigania chama hicho ili kiendelee kushika dola ndiyo lengo kubwa la umoja
huo na chama cha mapinduzi kwa ujumla.
‘’napenda niwaambie wajumbe mliochaguliwa,kama
kunamwanachama aligombea kwaajili ya kutafuta maslahi ya kiuchumi ni vizuri
akaachia ngazi kwakua sehemu kubwa tunajitolewa asiwepo mjumbe ambaye amefuata
maslahi’’ alisema.
Alisema kuwa UWT mkoa inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa
chama hicho kinashinda chaguzi mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika na kila
mwanajumuia hiyo anapaswa kutambua anafanya jitihada ya kuongeza wanachama
waaminifu watakao kuwa wakikichagua chama cha mapinduzi.
Awali akimkaribisha mwenyekiti wa umoja huo katibu wa UWT mkoa
Aziza Kiduda alisema kuwa taratibu zote zimefuatwa na wagombea nane wlijitokeza
katika kuwania nafasi tano zinazounda kamati ya utekelezaji ya jumuia hiyo.
Waliochaguliwa ni wajumbe wa baraza mkoa wa UWT ambao ndio
walipaswa kuwa wagombea wa nafasi ya kamati ya utekelezaji kwa mujibu wa katiba
ya umeoja huo.
Mwenyekiti wa umoja huo alimtangaza Ester Wafulukwizya,Rose
Chilumba,Mariam Seleman,Rehema Kauzeni pamoja na Mariam Meghji kuwa ndio
walioshinda katika uchaguzi huo na kuwa watakuwa wajumbe wa kamati hiyo kwa
miaka mitano ijayo.
Akitoa shukrani kwa wapiga kura mmoja wa washindi Ester
Wafulukwizya aliwashukuru wajumbe kwa imani kubwa kwa kuwachagua,na pia
aliwasihi wale ambao hawakuchagulia wasijioni kuwa hawafai kwani nafasi
zilikuwa tano na wagombea ni wanane hivyo lazima wengine wangekosa nafasi.
Alisema kuwa kilichopo ni kushikamana ili kukijenga chama
hicho kwani kila mmoja anawajibika kuhakikisha CCM inapata ushindi lakini kama
watajitokeza wa kuanzisha mivutano itasababisha kudhoofisha ushindi wa chama
hicho katika chaguzi mbalimbali zijazo.
Mwisho
0hermimyrrmu Michelle Lee https://wakelet.com/wake/Y6kMRfpxUs5BCmbzR1OZh
ReplyDeleteberbtebure
torla0cot-za-Fort Lauderdale Dereck Goon EaseUS Data Recovery Wizard
ReplyDeleteAdobe Audition
AVG PC TuneUp
orestworun
Ncersulsei_bo_2001 Donald Robinson Click
ReplyDeletesoftware
uneninel