Tuesday, 14 November 2017

Uharibifu wa mazingira wakwamisha kilimo cha umwagiliaji

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MRADI wa skimu ya umwagiliaji ya Ng'ongo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa unazidi kupungua uwezo wakuzalisha mazao siku hadi siku kutokana na ukosefu wa maji pamoja na wafugaji wanaofuchungia mifugo katika eneo hilo.

Akizungungumza jana mbele ya mkuu wa mkoa wa Rukwa mwenyekiti wa mradi wa scheme ya umwagiliaji ya Ng'ongo Justine Amon alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 wakulima waliweza kulima hekta 128 nakufanikiwa kuzalisha tani 460.8 za mahindi.

Alisema kuwa katika msimu wa mwaka 2016/2017 katika hekta hizo 128 uzalidhaji umeshuka hadi kufikia tani 358.4 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo haribifu wa mazingira pamoja na wafugaji kuchungia ndani ya eneo la uzalishaji. 

Amon alisema kuwa eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 630 lakini zinazolimwa ni hizo 128 tu kwakua ujenzi wa mfereji wenye urefu wa mita 3,000 haujakamilika kwa muda mrefu sasa.

Alisema kuwa mpaka sasa mfereji uliokalimilika unaurefu wa mita 1,725 ambao ndiyo unatumika katika umwagiliaji wa hekta hizo 128 ambazo wakulima wanafanya kilimo cha umwagiliaji mara mbili kwa mwaka ambao ni wa vijiji vya Ng'ongo,Mwela na Mtowisa. 

Mwenyekiti huyo alisema wakulima wanaolima kwenye eneo hilo wanalima zaidi mahindi,mpunga,nyanya na vitunguu ambapo wangenufaika zaidi iwapo mradi huo unge kamilika kwani wapo baadhi ya wananchi wanatamani kulima wanashindwa kutokana na kutokamilika kwa mradi huo. 
 
Alisema wa hisani walitoa shilingi milioni 600 ili kujenga mradi huo uwanufaishe wananchi lakini waliowengi wameshindwa kunufaika kutokana na mradi huo kutokamilika kwamuda mrefu hivyo wanaiomba halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga itafute fedha ili kukamilisha mradi huo.

Kwaupande wake mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alisema kuwa iliuzalishaji uweze kuongezeka ni lazima sheria ndogo za halmashauri zitumike kuwabana waharibifu wa mazingira. 

Alisema kuwa bonde la ziwa Rukwa limeelemewa na mifugo maratatu zaidi ya uwezo wake na hivyo Aliwataka wafugaji wapunguze mifugo kwa atakayeshindwa kukubaliana na agizo lake basi aondoke mkoani Rukwa akatafute sehemu watakayo mpokea. 

Mwisho

No comments:

Post a Comment