Na Walter Mguluchuma
Katavi
MAHAKAMA ya mwanzo wilayani Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu aliyekuwa akijitambulisha ni mwakilishi wa televisheni ya Star Tv mkoani humo pia mtoto wa Kamanda mstaafu wa Jeshi la polisi Sulemani Kova anaejulikana kwa jina la Gerald Kova mkazi wa mkoa wa Mwanza kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la uapateli.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Marko Pagyo baada ya kulidhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Awali mwendesha mashtaka wa jeshi la Polisi Wp Salma alidai Mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo februari 8 mwaka huu katika eneo la hotel ya Madina katika Manispaa ya Mpanda.
Alidai kuwa mshitakiwa huyo alijipatia kwa njia ya udanganyifu Kamera moja aina ya Canoni yenye thamani ya shilingi 3,500,000 pia computer aina ya Laptop pamoja na stendi ya Kamera ya video mali ya Elias Mlugala.
Alisema mtuhumiwa baada ya kujipatia mali hizo kwa njia ya udanganyifu alitoroka wilayani Mpanda na kutokomea kusiko julikana.
Alisema vitualivyotapeli ni camera aina ya Nikon D 7,200 mali ya Chama cha Wandishi wa habari mkoa wa Katavi yenye thamani ya shilingi 4,900.000.
Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kuiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa baada ya kutokomea haikujulikana alikokimbilia mpaka mwezi Agosti alipokamatwa huko Kahama ambako alikuwa ajimetambulisha kwa jina la Crispin Masawe na alikamatwa baada ya kufanya amefanya utapeli mwingine na kujipatia Lap top moja ya mwandishi wa habari.
Alidai kuwa baada ya kukamatwa alifikishwa mahakama ya mwanzo ya Kahama na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu au kulipa faini ya shilingi 100,000 hata hivyo hakuweza kulipa na kwenda gerezani kutumikia kifungo.
Mwendesha mashta alieleza ndipo waandishi wa habari wa mkoani katavi Elias na Kibada waliotapeliwa na mtuhumiwa huyo walipoa taarifa kituo cha polisi cha Mpanda juu ya mtuhumiwa wao kuhukumiwa kifungo hivyo walifanya utaratibu na waliweza kwenda Kahama na kumlipia faini na kumtoa gerezani kisha akawa chini ya ulinzi wa polisi na kusafirishwa hadi Mpanda na alipofikishwa aliweza kuonesha vifaa vyote,ambavyo alimuzia mfanyabiashara mmoja wa huko wa majimoto wilayani Mlele mkoani humo.
Mshitakiwa Gerald Kova katika utetezi wake kabla ya kusomewa hukumu aliiomba mahakama imwachie huru kwa kile alichodai kuwa anakunywa dawa za kufubaza makali ya ukimwi ARVs na anamatatizo ya ugonjwa wa sikoseli pia mama yake mzazi ni mgonywa na anamtegemea yeye.
Baada ya utetezi huo hakimu Paragyo alisoma hukumu na kuamuru mshitakiwa atumikie kifungo cha mwaka mmoja jela na pindi atakapo toka gerezani atatakiwa kulipa shilingi 800,000.
Mshitakiwa huyo anatarajiwa kufikishwa tena mahakamani kwaajiri ya kesi ya pili ya kuiba kamera aina ya Nicon mali ya Chama cha waandishi wa habari ambapo kesi hiyo itasikilizwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment