Thursday, 27 July 2017

Mkuu wa mkoa wa Rukwa awashauli madiwani wa upinzani wachukue hatua

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MKUU wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven amewashauri madiwani wa vyama vya upinzani mjini Sumbawanga kuanza kutafakari kutokana na kile kinachotokea kwa madiwani wa upinzani katika maeneo mengine hapa nchini. 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven akizungumza na mama aliyejifungua katika wodi mpya ya wazazi katika kata ya Mazwi

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akichangisha fedha kwaajili ya chumba kitakachotoa huduma za uzazi kwa wakinamama wa kata ya Mazwi.
Alisema kuwa raisi wa awamu ya tano hana ugomvi na vyama vingine vya siasa yeye anachotaka ni maendeleo lakini anawaasa majirani hao kutafakari juu ya kinachotokea katika maeneo mengine hapa nchini. 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa akizindua wodi ya wazazi katika kituo cha afya cha Mazwi

"ndugu zangu madiwani rais wetu hana ugomvi na vyama vya upinzani lakini nawaasaninyi madiwani hebu anzeni kutafakari na kuchukua hatua ila naamini mnaona na mtatendea kazi."..Alisema
Alisema kuwa yeye anakabidhi jumla ya vitanda vya kujifungulia wakinamama 16, vitanda vya wagonjwa wengine 80 na mashuka 200 ambapo vitu hivyo vilitolewa na rais John Magufuli ila yeye anakabidhi kwa niaba yake na vitagawiwa katika halmashauri zote nne za mkoa huo kadiri ya mahitaji. 
Mkuu huyo wa mkoa alitoa wito kwa watumishi wa afya katika mkoa wa Rukwa kujituma katika kuwahudumia wananchi sambamba na kuwa na lugha nzuri ambayo itakuwa ni faraja kwa wagonjwa. 
Baadhi ya vitanda vya wagonjwa vilivyotolewa na rais Magufuli
Alisema kuwa wananchi wanapaswa kulipa kodi bila kutegea ndipo serikali itaweza kuwahudumia wananchi kikamilifu kwakuwa itakua na uwezo wa kifedha. 
Aidha mkuu huyo wa mkoa aliiagiza idara ya afya mkoani humo kuwa hataki kuona wakinamama wazazi wakilala chini kwa madai kuwa vitanda havitoshi kwani ni lazima jitihada zifanyike kukomesha kabisa suala hilo.  
Baadhi ya vitanda vya kujifungulia wakina mama livyotolewa na rais
Awali mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa Bonifas Kasululu alisema kuwa bado idara ya afya mkoani humo inamahimahitaji makubwa ili iweze kuwahudumia wananchi ipasavyo kwani ndiyo lengo la serikali kuboresha afya za wananchi.  
Wananchi wa kata ya Mazwi pamoja na watumishi wa kituo cha afya cha mazwi wakimsikiliza mkuu wa mkoa

Alisema kuwa pamoja na changamoto hizo lakini bado wanajitahidi kuwahudumia wananchi kwa kiwango walicho nacho nakuwasihi wananchi wa kata ya Mazwi kukitumia kituo hicho badala ya kukimbilia katika hospitali ya mkoa ambayo ni hospitali ya rufaa kwa mkoa wa Rukwa inaanza kuelemewa na wagonjwa. 
Mwisho

No comments:

Post a Comment