Monday, 1 May 2017

Wenye vyeti 'feki' kutoswa zawadi za mei mosi

Gurian Adolf
Sumbawanga

BAADHI ya watu waliokuwa watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ambao Leo walio teuliwa kupewa zawadi ama cheti cha ufanyakazi bora wamepoteza sifa hiyo kutokana na kuwa utumishi wao umesitishwa kwa kukosa sifa stahili kutokana na kuwa na cheti bandia.

Akizungumza na rukwakwanza.blogspot.com  mkurugenzi wa Manispaa hiyo Hamid Njovu alisema kuwa haiwezekani tena wakapata  chochote kutokana na kupoteza sifa za utumishi.

Alisema kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa watumishi wa umma kutunukiwa cheti na zawadi mbalimbali ikiwemo fedha kutoka katika idara na kwa mwajiri wao lakini wale wote ambao wapo katika orodha ya watu walio  gushi vyeti basi wamepoteza sifa hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa hata katika halmashauri yake wapo ambao walikuwemo miongoni kwa watumishi ambao wangepewa tuzo hizo katika sherehe za mei mosi ambazo  kimkoa zitafanyika katika mjini wa Namanyere wilayani Nkasi lakini hawatapata chochote kwakua si watumishi tena.

Alisema kuwa ikitokea wamekwenda watakuwa kama wageni tu wengine wanaohudhuria sherehe hizo lakini hawana  sifa za Kupewa chochote kwakua si watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga.

Njovu alisema kuwa tayari kamati ya kupendekeza wafanyakazi bora wameshateua wafanyakazi wengine ili wapewe tuzo hizo kwakua halmashauri hiyo ina watumishi wengi wanaojituma katika kuwahudumia wananchi.

Hata hivyo alitoa wito  kwa watumishi wa halmashauri hiyo kuhudhuria katika sherehe hizo kwani ni muhimu kwao na kuwapongeza wenzao watakao pewa  vyeti na tuzo mbalimbali kwani wanastahili licha ya kuwa wote ni watumishi wachapakazi ila  watakao pewa tuzo ni mfano tu kwa wengine.
Mwisho

4 comments:

  1. We manage your travel on all domestic and international routes for any airline, offering the best services by our professional and Airline Tickets, Airfares and Discount Flight Deals for the smart value. LIVE Travel Experts Avail.
    https://airlines-booking.online/delta-ticket-online/
    https://airlines-booking.online/delta-flight-ticket-cancellation/
    https://airlines-booking.online/delta-flights-tickets-customer-service/

    ReplyDelete
  2. The Epson EcoTank L3210 is a fantastic option for anyone looking for reliable, cost-effective printing. With its refillable ink tanks and high-volume output, it’s perfect for home or office use. Need help with your printer. Visit Easy Printer Help for expert support and solutions.

    ReplyDelete