Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MKUU wa jeshi la polisi nchini,IGP Simon Siro amewapongeza waandishi wa habari mkoani Rukwa kwa Kushirikiana na jeshi hilo kwa kuendelea kuelimisha wananchi juu ya kupinga vitendo vya mauaji yanayotokana na wivu wa mapenzi pamoja na imani potofu za kishirikina.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi mkoani humo mkuu huyo wa Jeshi la polisi alisema kuwa waandishi wa habari wanajitahidi kutoa elimu kupitia vyombo vyao na hivyo wamekuwa ni nguzo muhimu katika kukabiliana na mauaji hayo holela.
Alisema kuwa vyombo vya habari vinanguvu kubwa ya kuibadiri jamii hivyo basi wanawajibika kufanya hivyo kwani kazi hiyo nilazima ifanywe kwa pamoja na wasiachiwe polisi peke yao kwani watakwama.
"nawashukuru wanahabari kwa jitihada zenu katika kuelimisha wananchi ili waache kufanya mauaji, kwani mauaji mengi yaliyopo mkoani Rukwa yanasababishwa na wivu wa kimapenzi sambamba na imani za kishifikina"alisema
Alisema iwapo kutakuwa na ushirikiano wa kutosha huenda mauaji hayo yakapungua kwakua elimu ni kitu kikubwa na wanahabari wanaweza kuitoa kupitia vyombo vyao vya habari.
"ninaziona jitihada zenu kupitia vyombo vya habari daima muongeze bidii kwani vita hii ni ya pamoja, endeleeni Kushirikiana vizuri ni lazima tufikie lengo la kupunguza mauaji hayo, ambayo yamekuwa changamoto kubwa katika mkoa wenu" alisema
Awali kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alimueleza mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini kuwa mkoa huo upo vizuri katika hali ya Usalama tatizo kubwa ni mauaji yanayotokana na wivu wa kimapenzi na imani za Kishirikiana.
Jitihada zinafanyika kumaliza changamoto hiyo licha ya kuwa unahitajika muda mrefu na ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari wa mkoa huo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment