Na Walter Mguluchuma
Katavi
WANANDOA Adamu Mtambo(41) na mkewe Catalina Mtambo(39 )wakazi wa Kitongoji cha Kasekese B Kata ya Kasekese wilayani Tanganyika Mkoani Katavi wameuawa kwa kukatwa mapanga wakiwa wamelala chumbani kwao.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kasekese Ramadhani Ibrahimu alisema kuwa tukio hilo lilitokea Jana majira ya saa 6:45 usiku nyumbani kwao.
Akielezea tukio hilo alisema kuwa marehemu Adamu ambae alikuwa ni mfanya biashara anamiliki maduka mawili Kijijini hapo siku hiyo alifanya biashara ya kuuza duka kama ilivyo kawaida yake na baada ya muda wa kufunga duka ulipofika alifunga na aliingia ndani kulala yeye na mke wake.
Wakati wakiwa wamelala walikwenda wauaji hao ambao wanasadikiwa kuwa walikua watatu na walifyatua risasi tatu za bunduki hewani ilikuwatisha majirani ambao wangefika kutoa miaada, kisha kuvunja mlango na kuingia ndani ya chumba moja kwa moja walichokuwa wamelala wanandoa hao.
Afisa mtendaji huyo alisema baada ya kuingia chumbani waliwakuta wanandoa hao kitandani ndipo walipoanza kuwashambulia kwa kuwakata kata kwa panga katika sehemu za usoni na kichwani na kuwashambulia kwa kutumia malungu.
Wakiwa wanawapiga marungu mwanaume alijaribu kuwasihi waache na na kuwaeleza kama shida yao ni fedha yupo tayari kuwaonyesha mahali zilipo lakini hawakuacha ndipo walipoanza kupiga makelele ya kuomba msaada kwa majirani.
Alisema kutokana na kelele hizo ndipo watoto wa marehemu ambao nao walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo wakiongozwa na kaka yao aitwaye Charles waliingia chumbani kwa wazazi wao kwa lengo la kutoa msaada hata hivyo walishindwa baada ya kushambuliwa na watu hao kwa kupigwa marangu hali iliyowalazimu wakimbilie kwenye vyumba vyao vya kulala na kujifungua.
Hata hivyo Majirani walifika kwenye eneo hilo na kukuta mlango wa mbele ya nyumba ukiwa umevunjwa na walipoingia kwenye chumba walichokuwa wanalala marehemu hao waliwakuta wakiwa wamelala chini ya kitanda huku wakiwa na majeraha makubwa katika sehemu mbalimbali za miili yao huku damu zikiwa zimetapakaa chumbani na wauaji kutorokea kusikojulikana.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kasekese Happnes Bona alisema jitihada za kutafuta usafiri kwa ajiri ya kuwafirisha wanandoa hao kuwapeleka hospitali ya wilaya ya Mpanda zilifanyika na wakiwa njia walifariki.
Alisema toka amekuwa mwenyekiti wa Kitongoji hicho hajawahi kuona mauaji ya kutisha na yakikatili kiasi hicho kwani marehemu hao waliuawa kwa kukatwa katwa kama wanyama.
Kwaupande wake kamanda wa polisi polisi mkoa wa Katavi Damas Nyanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo nakuongeza kuwa miili ya marehemu hao imeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya wilaya ya Mpanda kwaajili ya uchunguzi.
Alisema polisi wanaendelea kuwasaka watu waliofanya tukio hilo ili wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma za mauaji hayo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment