Sunday, 1 October 2017

Waahidi kulinda wanyama

Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Mamlaka ya usimamizi wa  Wanyama  pori Tanzania  TAWA imeahidi kuendelea kukabiliana naujangiri pamoja na kudhibiti uvamizi wa  mifugo  na shughuli za kilimo  kwenye maeneo  ya mapori ya akiba na tengufu.
Hayo yamebainishwa Jana na Kaimu Mkurugenzi  Mkuu  wa TAWA  Dkt  James Mwakibara  wakati akifunga mafunzo ya jeshi usu kwa Maafisa 59 wa kutoka  TAWA  yaliokuwa yakifanyika  kwenye kituo  cha  mafunzo cha  Mlele  mkoani  Katavi.
 Alisema lengo la  mafunzo  hayo  ni kuwaandaa  watumishi  wa  TAWA  kufanya kazi  katika  mfumo  wa  kijeshi (paramilitary)  ili  kuboresha  utendaji  kazi  kwa kujifunza  mbinu  za kupambana  na ujangili ,kuimarisha  nidhamu  ya watumishi  na kuboresha  mtiririko  wa kutoa na  kupokea amri.
 Dkt Mwakibara alisema  katika  suala zima la  kuapambana  na ujangili,TAWA  inaendelea kushirikiana  na Taasisi za  uhifadhi  na  vyombo vya  dola  pamoja na  wananchi  katika  mapambano hayo.
  Alisema  kuwa  wanaelewa   jitihada   zinazofanywa na bodi ya mamlaka  hiyo kuhakikisha  wanapata zana za kufanyia kazi ikiwemo kupata  sheria  ya  Mamlaka  na  mpango kazi (Strategic  plan) utakao saidia  kuwapa  nguvu  katika kutekeleza kazi zao.
Dkt   Mwakibara  alisema   TAWA  ni  Shirika  kubwa  na lipo nchi  nzima  linamiliki maeneo ya  wanyama pori  makubwa  mara  mbili  zaidi  ya TANAPA  na mara 13 zaidi  Mamlaka ya hifadhi  ya  Ngorongoro NCAA.
Ukubwa  wa  eneo   hilo ni  mtaji  katika  uchumi  na uzalishaji ili kufikia  malengo  yaliowekwa wanapaswa kuwa wabunifu  kwenye  kuongeza  mapato  na kudhibiti  mianya  ya upotevu wa  mapato ya nchi .
Alifafanua kuwa katika  mwaka  wa  fedha  wa  2016 na 207  mamlaka  ilipanga kukusanya  jumala ya  shilingi   Bilioni  40  lakini zilikusanywa  shilingi Bilioni 36  kwa  hiyo ni  jukumu  lao  wote kuhakikisha  wanapandisha  mapato  ili  kuweza  kutimiza  malengo  na kuweza kutatua changamoto  za uhaba  wa vitendea kazi  na kuboresha miundo mbinu.
Naye Mwenyekiti  wa  Bodi ya  Wakurugenzi  ya  Mamlaka  ya usimamizi wa  wanyama  Pori  Tanzania  TAWA   Meja  jenerali  Mstaafu Hamis  Semfuko  alieleza  kuwa ni  mategemeo yake  kuwa  mafunzo  walipatiwa  maafisa hao wa  Kati wa  TAWA  yatawaongezea  nguvu  katika kupambana na  ujangili  na  changamoto nyingine  ikiwemo  matumizi  ya silaha za  kivita  katika ujangili  na uvamizi wa maeneo ya  hifadhi.
 Alisema katika kuboresha  ulinzi wa  rasilimali za nchi  katika  maeneo yaliyo chini ya bodi  ya Tawa ilisha  toa  agizo  kwa  Manejimenti  kuhakikisha kwamba  Ofisi zote  za wakuu  wa vituo  zinahamia  kwenye  maeneo ya  mapori  husika   badala ya kuwa mijini .
Mwakilishi wa  Mkurugenzi  Mkuu wa  Tanapa  ambae  ni  Mkuu wa  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi  Izumbe   Msindai aliwaka  watumishi  wanofanya kazi  kwenye  Hifadhi  na   mapori ya  akiba  pamoja na tengefu  waepuke  kujihusisha na  maswala ya  rushwa  kwani  wapo  baadhi ya  watumishi wamekuwa sio  waadirifu.
Kwaupande wake mkufunzi Mkuu wa   mafunzo  hayo  Mhifadhi  Fidelis Kapalata alisema  wahitimu  hao  wamepatiwa  mafunzo hayo kwa  muda wa   wiki sita na yamewajengea  utimamu  wa  mwili  na mbinu za  kupambana  ujangiri pia ujasiri  wa kujiamini  na  hari katika kulinda  rasilimaii za wanyama pori.
Mwisho

No comments:

Post a Comment