Sumbawanga
MKUU wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven ameagiza kuanza kufanyika vikao vya kamati ya maendeleo ya wilaya (DCC) kwani vimekuwa havifanyiki kwamuda mrefu hali inayonyima fursa ya kupata usha ulio mzuri kutoka ngazi ya wilaya.
Akifungua jana kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Rukwa(RCC) alisema kuwa kwa muda mrefu sasa vikao hivyo havijafanyika kwa kisingizio cha kutokuwa na posho kitu ambacho siyo sahihi.
Alisema kwa ngazi ya mkoa kikao hicho kimekuwa kikifanyika bila posho Lakini cha kushangaza kwa ngazi ya wilaya vikao hivyo havifanyiki.
"naagiza kuanzia sasa nilazima vikao hivyo vifanyike posho ya kikao isiwe kigezo mbona vikao vya RCC vinafanyika na kamahakuna posho,tunalipa pindi zinapopatikana, sasa sitaki kusikia kuwa hamfanyi vikao vya DCC kwa madai kuhakuna posho"alisema
Aliwasihi watumishi wa umma Kuongeza kasi katika kuwatumikia wananchi kwani dunia hivi sasa imebadirika lazima tukimbie wakati wengine wanakimbia mkoa wa Rukwa unahitaji maendeleo kwa kasi kubwa.
Katika kikao hicho mmoja wa wajumbe waalikwa Zeno Nkoswe alipendekeza kuwa imefika wakati sheria iliyoanzishwa kuanzisha kikao hicho cha itazamwe upya uwakilishi uongezwe kwani wajumbe halali ni 28 ambao wanawakilisha wakazi zaidi ya milioni 1 wamkoa huo.
Nkoswe alisema kuwa kutokana na zama tulizonazo nivema idadi ya wajumbe wakikao hicho ikaongezeka kwa uwakilishi, tofauti na sasa walio wengi ni waalikwa ipo siku wanaweza wasije kwakua hawabanwi na sheria.
Pia alisema kuwa wakulima wamekata tamaa kutokana na kutokuwa na soko la zao la mahindi kwani wakulima wa mahindi hawana kwa kuyauza,wanakabiliwa na hali ngumu kiasi kwamba mkulima anaona kama kazi hiyo ni laana kutokana na ugumu wa maisha na hata wakiyauza humu nchini wanayauza kwa shilingi 40,000 kwa gunia bei ambayo haiwalipi.
Kwaupande wake Askofu wa kanisa la Moravian Dayosisi ya Sumbawanga Conrad Nguvumali alisema kuwa hivi sasa wakulima wamegeuka kuwa wafanyabiashara ya magendo kwaku waserikali imezuia kuuza mahindi nje ya nchi badala yake wakulima wanayatorosha mahindi nyakati za usiku kwakutumia punda na baiskeli.
Naye Mbunge wa Nkasi kusini Desderius Mipata alise makuwa mvua zimeanza kunyesha na mawakala bado hawajalipwa madeni yao huwenda wakashindwa kusambaza pembejeo kwa wakulima.
Alisema kuwa hali ya mawakala ni mbaya sana wengi wamefilisika na nyumba zao zinapigwa mnada na mabenki kutokana na mikopo waliyochukua kufanya kazi hiyo hivyo serikali iwalipe ili kuwakomboa.
Naye Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ally Kessy alisema kuwa vituo vya hali ya hewa vina majengo mazuri lakini sio msaada kwa wakulima kwani havitoi taarifa ya hali yahewa ipasavyo kwa wakulima.
Mwisho
No comments:
Post a Comment