Thursday, 16 November 2017

Jela kwa kubaka

Na Israel Mwaisaka
Nkasi
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30  Jela,kulwa Dase (35) mkazi wa kijiji cha Paramawe wilayani Nkasi kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 15.
Akisoma hukumu hiyo jana hakimu mkazi wa mahakama hiyo Ramadhan Rugemalila alisema kuwa mahakama imeridhishwa pasipo kuacha shaka yoyote na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hivyo kumuhukumu mtuhumiwa kifungo hicho.
Alisema kuwa kufuatana na mwenendo wa kesi hiyo ambapo mashahidi wanne waliweza kutoa ushahidi upande wa mashitaka  mtuhumiwa alikutwa na hatia chini ya kifungu cha sheria f namba 130(1) na namba (2)(e) NA 131 sura ya 16 ya kanuni ya  adhabu.
Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi Hamimu Gwelo uliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 12 mwaka huu majira ya saa 8 mchana.
Aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine baada ya vitendo kama hivyo kukithiri  katika siku za hivi karibuni.
Mahakama hiyo ilipompa nafasi ya kujitetea mtuhumiwa aliomba mahakama isimpe adhabu kali kwa maana hilo ni kosa la kwanza kwake na anategewa na familia yake.
Baada ya utetezi huo mahakama iliamua kutoa hukumu ya kwenda jela miaka 30.
Mwisho

No comments:

Post a Comment