Thursday, 12 October 2017

Matuta ya barabarani yalalamikiwa

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MKUU wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa ameishauri wakara wa barabara nchini Tanroads mkoani Rukwa kupunguza idadi ya matuta yaliyopo barabarani kati ya Sumbawanga mjini na kijiji cha mkutano ambacho ndio mpaka wa mkoa wa Rukwa na Songwe kwani imekuwa nichanzo  cha ajali.

Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya barabara mkoa wa Rukwa alisema kuwa katika barabara hiyo ya Sumbawanga Mbeya matuta yamezidi kiasi kwamba yamekuwa nikero. 

Alisema kuwa katika kipande hicho cha barabara chenye urefu wa kilomita 150 kinamatuta 139 ambayo ni mengi na nihatari kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kwani yamezidi kiwango. 

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa ajali nyingi zimekuwa zikitokea kwani matuta hayo yamekuwa yakichangia magari kupoteza muelekeo nivizuri ya kapunguzwa kwa usalama wa watumiaji wa barabara.

Naye mwenyekiti wa wakandarasi mkoa wa Rukwa Anyosisye Kiluswa alisema kuwa imefika wakati wakandarasi wazalendo wa anzekupewa kazi za daraja la 7 mpaka la tano kwani kazi hizo wamekuwa wakishindania na makampuni makubwa na yamekuwa yakishinda hivyo wakandarasi wazawa kukosa kazi na kushindwa kuchangia pato kwa kulipa kodi.

Alisema Tanroads itoe upendeleo maalumu kwao na makampuni makubwa yapewe kazi za daraja la 4,3,2 na kuendelea ambazo zinahitaji mitaji mikubwa na teknolojia kubwa ambayo wakandarasi wazawa hawana uwezo nazo. 

Mwenyekiti huyo alisema kuwa inapotokea barabara za mkoa huo zinapo haribika wanapewa wakandarasi wadogo kuzifanyia ukarabati hivyo kujikuta hawana mitaji yakufanya kazi hizo kutokana na kutopata kazi. 

Naye mbunge wa jimbo la Kwela Ignas Malocha alichangia katika kikao hicho alisema kuwa bado barabara za mkoa huo zinakabiliwa na changamoto ya wafugaji kupitisha mifugo yao barabarani kwa kuiswaga badala ya  kuipakiza katika malori. 

Alisema kitendo hicho kinasababisha uharibifu mkubwa wa barabara na kikiendelea kufumbiwa macho kitaendele kuharibu miundombinu hiyo.

Kwaupande wake mkuu wa mkoa huo ambaye pia ndiyo mwenyekiti wakikao hichoaliwaagiza Tanroads pamoja na TARURA mkoani humo kuhakikisha barabara zinakuwa bora wakati wote na kupitika bila usumbufu ikiwa ni pamoja na kuanza kufikilia barabara mbadala ili kuanza kujipanga kukabiliana nafoleni za magari siku zijazo.

Mwisho

No comments:

Post a Comment