Na Gurian Adolf
Katavi
MKE wa mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Katavi (CCWT) ameuawa kwakukatwa mapanga nakupigwa risasi tano kifuani akiwa nyumbani kwake na watoto wake wakiangalia televisheni.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Suzana Kabushi(40) Mkazi wa Kitongoji cha Msikitini katika Kijiji cha Kapanga wilayani Tanganyika mkoani humo.
Mume wa marehemu huyo Mussa Kabushi ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa mkoa wa Katavi alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya 2:00 usiku nyumbani kwa marehemu.
Alisema siku ya tukio marehemu alikuwa nyumbani kwake akiwa na watoto wake wanne wakiangalia TV mara baada ya kuwa wamekula chakula cha usiku wakati Mussa Charles akiwa ameenda katika kitongoji cha Center kwa ajili ya matembezi.
Wakati mwanamke huyo akiendelea kuangalia TV walitokea watu watatu wasiojulikana na kubisha hodi kwenye nyumba yao ndipo pasipo shaka aliweza kukalibisha akijua kuwa ni mume wake.
Kabushi alieleza kuwa mara baada ya kuwa wamekaribishwa alidhangaa kuona kuwa siyo mume wake bali ni watu asiowafahamu ambapo watu hao walimuomba marehemu awapatie maji ya kunywa kwa kile walichodai kuwa wanajisikia kiu ya maji kwani walikuwa wametembea kwa miguu kwa umbali mrefu.
Suzana ambae alikuwa amemshikilia mtoto wake wa kike mwenye umri wa miezi mitano alilazimika kumulaza kwenye kiti mtoto wake huyo na kisha kwenda kuwachukulia maji ya kunywa kwenye mtungi na kuwapatia.
Alisema mara baada ya kuwa wamekunywa maji hayo watu hawakumuuliza chochote na ndipo walipompiga risasi tano kifuani na kisha walikimbilia kusiko julikana.
Majirani walifika eneo hilo baada ya muda mfupi ndipo walipompigia simu mume wa marehemu na kumueleza kuhusiana na tukio Hilo kwa ndipo pia walitoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji ambao walitoa taarifa kwa jeshi la Polisi.
Polisi mara baada ya kufika kwenye eneo hilo na kufanya ukaguzi waliweza kuokota maganda sita ya risasi za bunduki ya SMG ambayo ndio ilitumika kufanya mauaji ya mwanamke huyo.
Mganga Mkuu wa Hositali ya Manispaa ya Mpanda Theopista Elias alisema mwili wa marehemu huyo umehifadhi katika chumba cha kuhifadhi maiti na mara baada ya uchunguzi wa kidaktari watakabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajiri ya mazishi .
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Damas Nyanda alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na polisi wanaendelea na msako kwalengo la kuwatafuta waliohusika na mauaji hayo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment