sumbawanga
MAJOKOFU ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Rukwa yameharibiribika kwa zaidi ya mwezi mmoja hivi sasa.
Kutokana na hali hiyo kumeleta usumbufu na gharama kwa baadhi ya ndugu wa marehemu ambao wanapenda kuhifadhi miili ya marehemu ili kuwasubiri ndugu wengine waliombali wafike kwaajili ya kuhudhuria maziko.
Mmoja wa wakazi wa mji wa Sumbawanga Maria Kayanda ambaye mjomba wake alifariki dunia Siku chache zilizopita alisema kuwa walilazimika kufanya maziko haraka kutokana na kushindwa kupeleka mwili wa mjomba wake huyo baada ya kupata taarifa kuwa majokofu ya chumba cha kutunzia maiti yameharibika.
Alisema kuwa mjomba wake alifariki usiku na wakafanya maziko siku iliyofuata lakini wao walitamani kuwasubiri ndugu zao wengine waliopo nje ya mji wa Sumbawanga na mkoa wa Rukwa lakini walishindwa na hivyo kulazimika kuzika.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alifika katika nyumba ya kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo nakufanikiwa Kuongea na mmoja wa wa wafanyakazi wa Mochwari kwasharti la kutokuandikwa jina lake gazetini kwamadai kuwa si msemaja ambaye alikiri kuharibika kwa majokofu hayo kwa muda wa mwezi mmoja na nusu hivi sasa.
Alisema jitihada za kuyatengeneza zilifanyika ambapo uongozi wa hospitali hiyo ulileta mafundi na walifika na mota nzima za majokofu hayo lakini baada ya kuzifunga hazikufanya kazi na wakazifungua na kuondoka nazo ambapo mpaka sasa hatujui nini kinaendelea.
"kutokana na kuwepo kwa hari hiyo miili marehemu imekuwa inahifadhiwa kwa kutumia kemikali aina ya fomalini ambayo huwa inatumika kuhifadhi maiti zisiharibike" alisema
Kwaupande wake kaimu Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Rukwa Emanuel Matika alikiri kuharibika kwamajokofu hayo ambapo alisema kuwa wao kama uongozi wametoa taarifa TEMESA lakini kwakua hawanafedha ndiyo maana hayaja tengenezwa bado.
Alisema hivi sasa utaratibu waTEMESA ni lazima walipwe fedha ndipo watengeneze na mchakato unaendelea watakapo pata fedha wata tengeneza.
Dk Mtika alisema kuwa kutokana na kuharibika kwa majokofu hayo kwa ndugu ambao wanasafirisha miili ya ndugu zao wanatumia dawa aina ya fomalini ili kuitunza isiharibike.
Mwisho
No comments:
Post a Comment