Wednesday, 11 October 2017

CCM wafuta uchaguzi

Na Walter Mguluchuma
Katavi
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi kimetengua matokeo ya uchaguzi ya nafas ya Mwenyekiti wa  CCM wa wilaya ya Tanganyika na nafasi ya Katibu wa siasa na uenezi pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya kwamadai kuwa msimamizi wa uchaguzi alikiuka kanuni za uchaguzi

Katika uchaguzi huo Yasin Kibiriti alitangazwa mwenyekiti wa  wilaya baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.
Uamuzi wa kutengua matokeo  hayo ulifanyika   juzi katika kikao  maalumu  cha  kamati ya siasa  ya  halmashauri kuu ya  CCM Mkoa wa  Katavi  kilichofanyika  katika ukumbi wa   idara ya  Maji  kilichoongozwa na  Mwenyekiti wa Ccm  Mkoa wa   Katavi  Mselemu   Abdallah.
Katibu  wa  Ccm wa  Mkoa Kajoro Vyohoroka  aliwaambia wandishi wa  Habari jana ofisini kwake kuwa  kikao  hicho  kilipokea  malalamiko ya  uchaguzi  wa CCM  Wilaya ya Tanganyika kwa  nafasi ya  Mwenyekiti  wa Wilaya  ambapo uchaguzi wake ulifanyika  terehe 10 oktoba  na  Yasin Kiberiti  alitangazwa na  msimamizi mkuu wa  uchaguzi huo kuwa ndiye  mshindi.
 Alisema kikao hicho  kilbaini kuwa  ni  kweli  kwenye uchaguzi huo  kanuni  ya uchaguzi  ilikiukwa  na msimamizi  mkuu  l Crisant Mwanawima  ambae   alikiuka  kanuni  ya uchaguzi  ya mwaka 2012 ibara ya 11b.
Aidha ibara  ya  21  b  ya  kanuni inaeleza kwamba   mshindi katika uchaguzi  kwa wagombea wasio  kundini  lazima  mshindi  atakae tangazwa  awe  amevuka  zaidi ya nusu  ya  kura zote zilizopigwa .
Kajoro alifafanua kuwa  kwa matokeo  yaliotangazwa  siku  hiyo ya  na msimamizi  mkuu wa  uchaguzi yalikuwa  kura halali zilizopigwa zilikuwa 458 kura halali  450 na kura  zilizoharibika  8 ambapo  Yasin  Kiberiti  alipata kura  222 Abdallah Sumry  kura  176 na  Mombo  Rashid  Mombo kura 55.
Alisema kwa   mantiki hiyo  kikao  kiliamua  kutegua  matokeo yote ya uchaguzi  ya wilaya  ya  Tanganyika  kwa  nafasi ya  Mwenyekiti wa  Ccm Wilaya ,Katibu  wa siasa   na uenezi  wa  Wilaya  na wajumbe  wote  wa  kamati  ya siasa  ya Halmashauri  kuu ya Ccm  Wilaya.
Katibu  huyo wa  CCM  wa  Mkoa  alizitaja  sababu zilizopelekea  kutengua kwa matokeo ya umshindi wa  Mwenyekiti kuwa  ni  mshindi  kwenye uchaguzi huo hakupata zaidi ya nusu ya kura  halali  zilizopingwa  kwa mujibu  wa kanuni  ya uchaguzi .
Kikao kilichotengua matokeo hayo kilibaini kuwa  msimamizi mkuu  wa uchaguzi kabla ya kutangaza  matokeo  hayo   yawezekana  alifanya  kwa makusudi  kwa lengo la kumbeba  mgombea  mmoja  na ndio maana  hakumshirikisha  msimamizi  msaidizi wa uchaguzi  wala mkurugenzi wa uchaguzi wa  wilaya  hiyo.
Alisema   kwakuwa   Mwenyekiti  alitangazwa  mshindi kinyume  na  kanuni za  uchaguzi  ndani ya  chama  hivyo  hivyo  hata kikao cha  Halmashauri kuu  ya  Ccm alichokiongoza baada ya kuchaguliwa  nacho kilikuwa ni  batili  hivyo matokeo ya  Katibu  na uenezi  pamoja  na  wajumbe wa   kamati ya siasa ya  Wilaya  nao  uchaguzi wao umefutwa.
Kuhusu  adhabu aliyopewa  msimamizi  huyo wa  uchaguzi, Kajolo  alisema  amepewa  adhabu  kwa mujibu  wa  kanuni za  chama  za uongozi  na maadili  kwa kushindwa kwake  kusimamia  vema uchaguzi huo  huku  akiwa  anajua  kuwa   anavunja  kanuni ya uchaguzi.
Mwisho

No comments:

Post a Comment