Katavi
Meya wa Manispa ya Mpanda Willy Mbogo amekanusha uvumi unaoenea katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Katavi kuwa ameanza mikakati ya kumng'oa mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi katika uchaguzi mkuu ujao
Mbogo ambae ni Diwani wa Kata ya Kashauli kupitia CCM alisema hayo jana wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Majengo katika uzinduzi wa kisima cha maji kilichojengwa na Kampuni ya kuuza mafuta ya GBP kilichogharimu kiasi cha shilingi Milioni 55 ikiwa ni msaada uliotolewa na Kampuni hiyo.
Alisema kuwa amekuwa akizushiwa kuwa anampango wa kugombea ubunge katika Jimbo hilo kitu ambacho sikweli kwani mpaka sasa hana mpango wowote wakugombea ubunge katika jimbo lolote mkoani humo.
Alisema kuwa yeye binafsi anapenda kuwahakikishia wakazi wa Manispaa ya Mpanda na wananchi wa mkoa wa Katavi kwa ujumla kuwa hana mpango wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2020 kwenye jimbo lolote la Mkoa wa Katavi.
Alisema kuwa nafasi ya udiwani aliyonayo inamtosha hivyo ataendelea kuwatumikia wananchi katika nafasi hiyo kwani inamfanya kila siku kufanya kazi ya kuwatumika wananchi kwa karibu zaidi.
"nimekuwa nikuzushiwa mara kwa mara kuwa nampango wa kugombea udiwani,hata hivi karibuni wakati wa mkutano mkuu wa CCM wa Wilaya ya Mpanda baadhi ya wajumbe wa mkutano huo walihoji swala hilo" alisema
Alisema ameamua kukanusha mapema kwani anaona siku hadi siku watu wanaendelea kuzusha kitukisicho moyoni mwake kwa sasa wala hafikikii kabisa zaidi ya kuendelea kuwatumukia wananchi wake kwa nafasi ya udiwani.
Alieleza kuwa wakati wa mkutano Mkuu wa uchaguzi uliofanyika yeye aligombea ujumbe wa mkutano mkuu wa Taifa na alishinda hivyo watu ambao walikuwa wameanza kumzushia kuwa kwanini agombee nafasi hiyo wakati pia anampango wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment