Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WAKAZI
katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wanaendelea na zoezi la kujiandikisha
katika Daftari la kudumu la wapiga kura kazi ambayo imeanza tangu majira ya saa
2;00 za asubuhi ya leo.
Watu
wamejitokeza katika vituo vya kuandikishia kwaajili ya kujiandikisha ili waweze
kupata fursa ya kushiri uchaguzi mkuu
mwezi oktoba mwaka huu ambapo itakuwa ni uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais.
Akizungumza na Ndingala Fm muda mfupi uliopita
Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Himid Njovu amesema kuwa mpaka hivi
sasa zimejitokeza changamoto ndogo ndogo kama vile mashine kuweka kumbukumbu za
mtu aliepita na hivyo kila mara kuzirudia kumbukumbu hizo lakini tayari wamesha
tatua hali hiyo.
Kwa mujibu
wa Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga amesema kuwa taratibu zote
zimekwisha andaliwa na kila mtu mwenye sifa ya kupiga kura atapata fursa hiyo
bila hofu yoyote.
Amesema
iwapo kutajitokeza changamoto yoyote wamejipanga kukabiliana nayo na katika
kituo chochote ambacho kutakuwa na changamoto hiyo watoe taarifa haraka ili
kutosababisha kusimama kwa zoezi hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 23 Mei 2015 kuelezea juu zoezi la uandikishiaji wa Wananchi kwenye daftari la kudumu la Mpigakura lililoanza rasmi leo tarehe 24 Mei 2015 Mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
No comments:
Post a Comment