Wednesday, 11 October 2017

B. O. T yawapiga msasa viziwi

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WATU wenye ulemavu wakusikia(viziwi)mkoani Rukwa wameishukuru Benki kuu ya Tanzania kwa kuwapa mafunzo maalumu ambayo yamewajengea uwezo wa kutambua namna bora ya kuhifadhi fedha sambamba na kujua tofauti ya fedha halali na bandia.

Mafunzo hayo  ya siku moja yaliyofanyika jana katika ukumbi wa Moraviani Conference yalihusisha watu wenye ulemavu wakutosikia ambapo walifundishwa namna bora yakuhifadhi fedha pindi waendapo katika matumizi kwani watu wengi wamekuwa hawajui namna bora ya kuweka fedha zao. 

Akizungumza katika Mafunzo hayo meneja msaidizi idara ya  Benki kuu Tanzania Vick Msina,alisema kuwa watu wengi wamekuwa hawajui namna bora bora ya kuweka hela kwani wamekuwa wakizikunja nakuziweka mifukoni ama wanawake kuzifunga katika kanga walizo vaa kitendo kinacho sababisha hela hizo kuchakaa mapema.

Alisema ni vizuri mtu yeyote anapokuwa anakwenda kufanya manunuzi akawa anabeba hela kwenye pochi zikiwa zimenyooka badala ya kuzikunja na kuweka mfukoni,ana kuweka miguuni kwenye soksi ama kwenye sidiria kwani kufanya hivyo kunasababisha hela kuchakaa haraka. 

Huyo alisema kuwa suala hilo si tu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia bali ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa ana zitunza fedha vizuri ili zitumike kwa muda mrefu. 

Naye mwenyekiti wa viziwi mkoa wa Rukwa Henry Kisusi alisema kuwa mafunzo hayo yamekuwa nimuhimu sana kwao kwani wamekuwa hawapati fursa nyingi na hivyo kujikuta wakitumia vibaya fedha hizo pamoja na kubambikiziwa fedha bandia.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo mwenyekiti wa kituo cha viziwi nchini Habib Mlope alisema kuwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wakiwemo viziwi wanatakiwa kupewa mafunzo mara kwa mara yatakayo wasaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali hususani katika zama hizi ambazo baadhi ya watu wanapenda kuendesha maisha kwanjia ya utapeli. 

Mwisho

No comments:

Post a Comment