Friday, 8 September 2017

wanaswa na meno ya tembo

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
JESHI la polisi Mkoani Rukwa limefanikiwa kuwakamata watu wanne wakazi wa kijiji cha China kilichopo katika pori la akiba la Lwafi wilayani Nkasi mkoani Rukwa wakiwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilogramu 9.25 yenye thamani ya shilingi milioni 67.

Tukio hilo lilitokea Septemba 7 majira ya saa  09.00 za mchana huko katika kijiji cha China, ndani ya pori la akiba la Lwafi, Barabara ya  Kitosi Wampembe, kata na tarafa ya Kate,wilaya Nkasi Mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo kamanda wa polisi mkoani humo George Kyando alisema kuwa  kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na msako uliofanyika kati ya askali Polisi wa wilaya ya Nkasi na askari wa Wanyamapori huko wilayani Nkasi.

Baada ya kufanya msako huo wa pamoja watu wanne walikamatwa ambapo wote  ni wakazi wa kijiji cha Mkangale Namanyere wakiwa na meno manne ya tembo yenye uzito wa kilo 9.250 ambayo yanathamani ya shilingi 
milioni 67,211,200.

Alisema mbinu iliyotumiwa na watuhumiwa hao ni kuyasafirisha  meno hayo kutoka kijiji cha Mkangale kwenda 
Katika kijiji cha Wampembe mwambao mwa ziwa Tanganyika kwa lengo la kuyauza na ndipo askari walipopata taarifa za kiintelijensia na  kuweka mtego wa kuyanunua na kufanikiwa kuwakamata.

Aidha meno hayo yalifungwa ndani ya mfuko wa Sulphate yakiwa yamechanganywa na miwa kwa kigezo kuwa wamebeba mbegu za miwa ili wasikamatwe na kuupakia` kwenye pikpiki yenye zenye namba ya usajili MC 484 AJN ikiendeshwa na Evans Tenganamba pamoja na abiria aliyejulikana kwa jina la Elisha John na Pikipiki  nyingine  MC 480 aina SANLG  ikiendeshwa na Justine Kapembwa ikiwa akiwa amembeba Sandu John.  

Kamanda huyo wa polisi alisema kuwa wamiliki wa meno hayo ya tembo ni Sandu John na Elisha John na ndio watuhumiwa wakubwa wa uwindaji haramu ambapo  wote kwa pamoja wanashikiliwa na polisi.

Mwisho

No comments:

Post a Comment