Mlele
ZAIDI ya kaya 80 zilizopo katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi zinalalamikia kubobolewa nyumba zao na kamati ya ulinzi nausalama ya wilaya hiyokwamadai Kuwa wamejenga nyumba hizo Katika eneo la mnada lililopo wilayani humo.
Kitendo hicho kimesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa kitongoji cha Kitupa kata ya majimoto wilayani humo hali ambayo baadhi ya familia zinalala nje kutokana na kukosa nyumba za kuishi huku wakipatwa na baridi kali ambayo inawezakuwasababishia ugonjwa wa Nimonia kwa watoto wadogo.
Akieleza tukio hilo la kubomolewa nyumba zao na askari wa polisi pamoja na askali wa Tanapa na Jeshi la akiba, mmoja wa wahanga hao Eliasa Chimbamawe alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa sita mchana.
Alisema yeye ni mzaliwa wa Kitongoji hicho na amekuwa akiishi kwenye eneo hilo toka mwaka 1949 pamoja na wazazi wake walifariki mwaka 1975 na makaburi yao yapo kweye eneo hilo linalodaiwa kuwa niIa mnada.
Naye Festo Lazaro alieleza kuwa yeye na familia yake walivamiwa na askari hao waliwalazimisha wabomoe nyumba yao na wakati wakiwa wanabomoa walilazimishwa kuimba nyimbo za hamasa kwaajiri ya kuwatia nguvu .
Alieleza kuwa baada ya kuwa wamebomolewa nyumba yao yeye na familia yake wamekuwa wakiishi kwa kuteseka na wamekuwa kama wageni kweye nchi yao wenyewe.
Anoneta Joseph alieleza kuwa kitendo cha kubomolewa nyumba yake kulisababisha watoto wake kunusurika kupoteza maisha kwani wao wako shuleni wanasoma Sekondari walipoambiwa kuwa nyumba yao imebomolewa walipoteza fahamu na kuzirai.
Alisema yeye eneo hilo alilokuwa akiishi alilinunua toka mwaka jana wakati akiwa na marehemu mume wake ambae alifariki mwaka huu na kumwachia watoto wanne ambao anaishi nao akiwa ni mjane .
Kwaupande wake Meda Shigela alisema yeye alianza kuishi kweye eneo hilo toka mwaka 1997 na baada ya kubomolewa yumba zake yeye mweye familia ya watoto 13 amelazimika kulala nje pamoja na wakwe zake na watoto wake kitu ambacho sio utamadui wao kuishi namna hiyo.
Aliiomba Serikali ione namna ya kuwasaidia kwani baadhi yao ni watu ambao ni wazee na mpaka sasa hawajui watakakokwenda na pia hata uwezo wa kujenga tena nyumba hawana.
Gwazo Sunde alieleza kuwa wakati anabomolewa nyumba yake aliambiwa kuwa nyumba yake inabomolewa kwaajiri ya kupisha mnada hivyo kwa sasa analala chini ya mti yeye na mke wake na mama mkwe wake huku wakihofia kuibiwa mali zake ambazo zipo nje na mbaya zaidi wamebomoa hata choo.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho cha Kitupa Mkamba Mzoloka alieleza kuwa ni kweli wakazi hao wamebomolewa nyumba zao ili kupisha upauzi wa mnada na taarifa za kubomolewa kwa nyumba hizo alizipata siku moja kabla ya tukio hilo kwa kupitia matagazo ya vipaza sauti.
Alisema ni vema kabla ya kubomoa kwa nyumba hizo wangekuwa wamewaandalia wananchi hao eneo jingine la kuishi kuliko walivyowabomolea na kuwaacha wasijue kwa kuishi wapi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment