Tuesday, 1 August 2017

Mwenyekiti wa CCM abwaga manyanga

Na Gurian Adolf
Katavi .
 MWENYEKITI wa   CCM  wa   Mkoa wa   Katavi  anaemalizia  muda   wake  mwaka huu   Mselemu  Abdalla   ameandika  barua ya  kujiondoa kugombea  nafasi  hiyo  licha  ya   hapo  awali kuchukua  fomu ya kugombea  nafasi  hiyo  kwakile kinachodaiwa kuwa ni  kutofauniana  na  viongozi  wenzake  kwenye kikao  cha   Halmashauri kuu ya CCM  ya  Mkoa huo.
 Akiongea  na  gazeti  hili  jana   Mselemu  alikiri  kuwa  nikweli ameamua kuandika barua ya  kujiondoa  kugombea  nafasi  hiyo na tayari amekwisha mkabidhi Katibu  wa  CCM   wa   Mkoa   wa   Katavi  nia yake hiyo.
 Alisema   nafasi  hiyo kwa  uchaguzi   wa  mwaka  huu   walichukua fomu ya kwa lengo la kuomba   kugombea  nafasi  hiyo  wagombea 12  hivyo baada kujiondoa yeye  katika anaamini hao  waliobaki  atapatikana kiongozi  mmoja   ambae   atakuwa  ni  bora.
Kwa  mujibu  wa  taarifa  za  ndani ya  kikao  cha   Halmashauri kuu  ya  CCM  Mkoa wa  Katavi kilichofanyika   wiki  iliyopita   katika   ukumbi wa    CCM  Wilaya ya   Mpanda  chanzo  cha   Mwenyekiti  huyo  kuamua  kuandika   barua ya   kujiondoa  kugombea  nafasi hiyo kumetokana na  kutofautiana  maamuzi  ya    wajumbe wa   kikao  hicho.
Inadaiwa  kuwa  siku  hiyo  kikao  hicho  kilichokuwa  kikiongozwa  na yeye  kilikuwa  kinawajadili na  kuwapitisha  majina  ya  wana  Ccm  waliokuwa  wakiomba   kuteuliwa  kugombea   nafasi mbalimbali  za  uongozi wa  Kata    katika   Kata mbalimbali za   Mkoa huo .
Mwenyekiti  huyo  alikuwa  hataki   baadhi ya  wagombea  majina  yao  yapitishwe  na  kikao  hicho wakiwemo  baadhi ya   viongozi wa  sasa  wanao toka  kwenye   baadhi ya   Kata  na  wengine  ambao yeye   alikuwa   amewasimisha  uongozi   licha  ya  viongozi  hao  kuwa  wamepewa   alamu   nzuri   na vikao  vya   kamati ya   siasa  kwenye   Wilaya  zao ambapo walipata sifa stahili za kuwa wagombea.
Chanzo   cha   habari  hizi  kutoka  ndani ya  kikao  kinaeleza  kuwa  miongoni mwa  viongozi  ambao  alikuwa  hataki  wapitishwe ni  Mwenyekiti wa   Kata   na Katibu wa   Kata ya  Majengo  na makatibu  wa   Kata  za   Mnyagala , Katuma ,   Uwanja wa  ndege , Maji  Moto na Kibaoni.
  Hata  hivyo   wajumbe wa  kikao  hicho walipinga  uamuzi wa  kuondolewa  majina  ya   watu  hao   hali  ambayo  ilimlazimu   mwenyekiti  huyo  kutamka kuwa  basi   majina  hayo  yarudishwe  kwenye  kikao  cha   Kamati ya   siasa ya  mkoa  kwa  ajiri ya kujadiliwa  upya   ombi   ambalo lilipingwa vikari na wajumbe wa kikao  hicho  kwa  kile  walichodai kuwa  kikao  hicho  cha  Halmashauri kuu  ndio  chenye   mamlaka na uteuzi na  sio  kamati ya siasa.
Baada ya  mawzo  yake   kupingwa  Mwenyekiti huyo  aliagiza  zipingwe  kura   na  wajumbe  wa  kikao hicho za  wanaunga  mkono   mapendekezo  yake  na wale  wasiounga  mkono  mapendekezo yake   na  katika  kura   zilizopingwa  wajumbe   9  walimuunga  mkono   na  wajumbe  19  hawakumuunga  mkono hivyo  mapendekezo yake  yakawa  pametupiliwa  mbali na   majina  ya wale  ambao  alikuwa  hawataki yakawa yamepitishwa.
 Kutokana na   kitendo  hicho  cha   kutoungwa  mkono  mapendekezo yake  yalimkasirisha   mwenyekiti huyo  na   kuamua  kuandika  barua ya  kujiondoa kugombea  kwa kuhofia kuwa  hata  kama    atashinda  kuwa  Mwenyekiti wa   Mkoa  upo uwezekano wa  kukosa  ushirikiano  kutoka kwa viongozi  wenzake ambao hakuwataka iwapo watapata ridhaa ya wanachama kwa kuchaguliwa.
Mwisho

No comments:

Post a Comment