Na Walter Mguluchuma
Katavi
MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Beatrice Kangu(48)Mkazi wa Mtaa wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amefariki Dunia ghafla muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya shukrani akiwa anasali ibada katika Kigango cha Makanyagio B mjini humo
Tukio la kifo hicho cha mwanamke ambae alikuwa ni muumini wa dhahebu la Romani Catoliki lilitokea hapo Julai 30 majira ya saa moja na nusu asubuhi katika Mtaa wa Makanyagio wakati wa ibada.
Kwamujibu wa makamu Mwenyekiti wa Kigango hicho Charles Kanyanda alieleza kuwa siku hiyo Kangu alifika kwenye ibada kwenye kigangoni hapo kama ambavyo walivyofika siku hiyo waumini wengine kwa ajiri ya kusali.
Alisema baada ya kufika alikwenda kujiunga na wanakwaya wenzake wa kwaya ya Kigango cha Makanyagio ambapo nae alikuwa ni miongoni mwa waimbaji wa kwaya kwenye ibada hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Katikisita wa Kigango hicho Agustino Ntalwila.
Ibada hiyo iliendelea kama kawaida na ndipo ilipofikia muda wa kutoa sadaka ambapi alikwenda kutoa sadaka kama kawaida na kisha kurudi kwenye kwaya na kuendelea kuimba.
Baada ya mahubiri ya Katekista Ntalwila ilifuata utoaji sadaka ya shukurani na ndipo mwanakwaya huyo alipoinuka alipokuwa amekaa na kwenda kutoa sadaka ya shukurani na baada ya kutowa sadaka hiyo alianguka chini ghafla.
Wanakwaya wenzake walijaribu kumpa msaada hata hivyo hali yake iliendelea kuwa mbaya na alifariki dunia baada ya muda si mrefu na kuacha simanzi kubwa kwa waumini wa kigango hicho.
Kanyanda alisema mazishi ya marehemu huyo yalifanyika jana katika makaburi ya Mwanga na misa ya mazishi iliongozwa na Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Maria Imakulata Monsinyori Padri George Kisapa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment