Na Walter Mguluchuma
Katavi
SHIRIKA la Reli Tanzania TRL limewataka limewataka watu waliovamia hifadhi za reli na kujenga nyumba za kuishi ndani ya hifadhi hizo kuzibomoa wao wenyewe kwa hiyari kabla shirika hilo halijafanya maamuzi ya kuzibomoa na endapo wakipuuza shirika hilo likibomoa itabidi walilipe shirika hilo kwa kufanya kazi hiyo ya kubomoa.
Mkurugenzi mkuu wa TRL hapa nchini Masanja Kadogosa aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa shirika hilo katika stesheni ya Mpanda Mkoani Katavi.
Alisema kuwa shirika hilo halitamvumilia mtu yoyote aliyejenga nyumba ndani ya hifadhi ya reli kuendelea kuishi kwenye eneo hilo kwani ilimetoa muda wa miezi sita wawe wamebomoa nyumba zao na kuondoka Mara moja
Meneja huyo aliwaonya watu hao kuwa endapo baada ya muda kupita mtu yoyote ambaye hatakua hajabomoa nyumba yake shirika litabomoa na gharama husika zitalipwa na mtu aliyejenga na kukaidi agizo la kubomoa.
Kadogosa alisema kuwa kwa yale maeneo ambayo shirika litaamua kujenga reli na kuwakuta wananchi wame jenga nyumba watu hao watalipwa fidia na shirika hilo.
Hata hivyo shirika hilo hivi karibuni lilitoa notisi ya kuwataka watu waliojenga nyumba katika maeneo ya Msasani na Tambukaleli katika Manispaa ya Mpanda pamoja na wakazi wa Kijiji cha Ugala Tarafa ya Nsimbo Wilayani Mpanda ambao wamejenga nyumba zao ndani ya hifadhi za reli kuhama na kubomoa nyumba zao ndani ya kipiindi cha siku 30.
Hata hivyo Naibu Waziri wa Ujenzi Edwin Ngoyani alipokuwa katika ziara hivi karibu Mkoani Katavi aliwaongezee muda wa kuishi kwenye maeneo hayo hadi mwezi januari mwakani.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRL Prof John Kondoro aliwataka watumishi wa TRL wawe wawazi kila wanapofanya kazi za kuwahudumia wananchi kama anavyofanya rais John Magufuli ambavyo hataki njia za mkato za kufanya kazi kwa ujanja ujanja.
Alisema shirika hilo halitakiwi kuwa mzigo kwa Serikali badala yake linatakiwa TRL kutoa ruzuku kwa Serikali.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nsimno Richald Mbogo alieleza kuwa tayari wananchi wa Kijiji cha Ugala mameanza kupimiwa viwanja kwa ajiri ya ujenzi wa nyumba zao ili waweze kuhama kwenye maeneo ya hfadhi ya reli.
Alisema yeye kama Mbunge wa Jimbo la Nsimbo amesha andika barua ya kumwomba Waziri wa ujenzi kuwaongezea muda wananchi waliokuwa wamejenga nyumba kwenye maeneo hayo iliwaweze kufanya maandalizi ya ujenzi kwenye maeneo waliotengewa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment