Monday, 17 July 2017

Nkasi waanza kupiga chapa ng'ombe wao

Na Israel Mwaisaka
Nkasi
MKUU wa wilaya ya NKASI  mkoani Rukwa Said Mtanda  amepiga marufuku utaratibu  unaotumiwa na baadhi ya watumishi wa idara ya afya wilayani humo wa kuwashirikisha wananchi kuchangia ununuzi wa mafuta ya gari la wagonjwa na pia posho ya dereva wa gari hilo
 Mtanda amesema hayo kwa nyakati tofauti katika kata za Kirando na Kabwe wakati wa kukabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa yaliyotolewa msaada na serikali na kuwa  watumishi watakaotuhumiwa  kujinufaisha kinyume cha taratibu za utumishi wa umma  kwa kuwatoza wananchi gharama za uendeshaji wa magari hayo  watawajibishwa 
alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa Wananchi ya kudaiwa fedha pale wanapohitaji huduma ya gari la wagonjwa na kuwa sasa wanakabidhi gari hilo ili liweze kutumika kuwasaidia wagonjwa na kuwa hataki kusikia tena malalamiko kama hayo.
mbunge wa jimbo la Nkasi kasikazini Ally Kessy kwa upande wake aliwataka wananchi katika maeneo hayo kuhakikisha kuwa wanayatunza magari hayo vyema na yanatumika katika kazi kusudia ili yaweze kudumu kwa muda mrefu na jamii waweze kunufaika ipasavyo.
alidai kuwa ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa mgonjwa anapata huduma ya gari pale inapohitajika bila ya kudaiwa chochote na kuwa wanananchi wawe wepesi kutoa taarifa pale wanapoombwa kutoa fedha za mafuta ili waweze kushughulikiwa.
Msaada wa magari hayo uliotolewa na serikali kwa ajili ya wananchi wa jimbo la Nkasi kaskazini umelenga kuboresha huduma ya afya kwa wananchi  wanaoishi katika  vijiji mbalimbali vya mwambao wa ziwa Tanganyika ambapo magari hayo ya kisasa ya yenye thamani ya zaidi ya shs milioni 300 yanatarajiwa kutoa huduma ya afya kwa  wakazi zaidi ya elfu 90 wanaoishi kwenye kata sita za mwambao wa ziwa hilo katika tarafa ya Kirando
mwisho

No comments:

Post a Comment