Na Walter Mguluchuma
Katavi
JESHI la polisi mkoani Katavi limemteua aliyekuwa OCD na aliyestaafu hivi karibuni wa wilaya ya Mpanda mkoani humo, Zeno Malesa kuwa mshauri wa maswala ya ulinzi na usalama wa Mtaa wa Kasimba katika Manispaa ya Mpanda kutokana na juhudi zake alizokuwa akizifanya za kupunguza matukio ya ujambazi pamoja na biashara ya ukahaba kabla ya kustaafu kwake kazi katika jeshi hilo katika wilaya hiyo.
Uamuzi huo wa kumteuwa Malesa kuwa mshauri wa masuala ya ulinzi katika mtaa huo ulifanywa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Damas Nyanda wakati wa sherehe za kumuaga mstaafu huyo na zilizofanyika katika ukumbi wa Neema uliko katika Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda.
Alisema OCD kuwa mstaafu huyo amelitumikia jeshi la polisi kwa uaminifu mkubwa kuanzia mwaka 1973 alipojiunga na jeshi hilo hadi Julai 1 mwaka huu ambapo ameweza kufanya kazi ya polisi kwa kipindi cha miaka 44 kwa uadilifu mkubwa.
Alifafanua kuwa kwa kipindi alichoongoza Wilaya ya Mpanda amefanya kazi nyingi mbalimbali za kupambana na uharifu na ameweza kupunguza matukio ya ualifu kwa kiasi kikubwa.
Pia ameweza kupunguza matukio ya biashara ya ukahaba na matukio kumi kwa kipindi cha mwaka jana hadi kufikia matukio matatu kwa kipindi cha mwaka huu wa 2017.
Nyanda alieleza kuwa kutokana na mchango wake huo mkubwa katika jeshi la polisi ndio maana ameamua kumteuwa kuwa mshauri wa maswala ya ulinzi na usalama katika mtaa anao ishi wa Kasimba iliaendelee kutoa mchango wake kwa jeshi la polisi.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Kamishna wa Polisi Paulo Chagonja alisema kuwa jeshi la polisi linajivunia mafanikio ya OCD huyo mstaafu na atakuwa ni daraja kati ya polisi na raia na Balozi.
Alisema ukiona mtumishi wa jeshi la polisi ameweza kufanya kazi na kufikia ngazi aliyokuwa nayo Malesa ujue kuwa mtu huyo alikuwa ni mwadilifu na ndio maana jeshi la polisi lilimwamini.
Kwaupande wake mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Mpanda ambae pia ni mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga alisema kuwa hali ya matukio ya uharifu kwa wilaya ya Mpanda yamepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano ulipo baina ya polisi na wananchi hivyo alimtaka ocd aliyehamishiwa kwenye Wilaya hiyo kuendeleza ushirikiano na mahusiano na wananchi kama uliokuwepo hapo awali.
Mwisho
.
No comments:
Post a Comment