Na Israel Mwaisaka
Nkasi .
SERIKALI ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imeziamuru Serikali za Vijiji na Kata wilayani humo kuwatumia askari mgambo maarufu askari wa akiba kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao ili kukabiliana na visa vya mauaji vinavyofanywa na wananchi wanaojichukulia sheria mikononi kila kukicha .
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda ambaye pia kwa wadhifa wake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kufuatia malalamiko ya visa vya kihalifu ikiwemo mauaji yanayofanywa kiholela na wananchi yaliyotolewa na baadhi ya madiwani katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana mjini Namanyere wilayani hapa .
“Ni kweli hali ya ulinzi na usalama katika baadhi ya vijiji wilayani hapa sio ya kuridhisha kumekuwa na visa vya unyanyasaji , ukatili , ubakaji na mauaji yanayotokea kila kukicha ambayo nieleze wazi yanafanywa na watu wa jamii ya wafugaji ….
Sasa naa agiza Serikali za Vijiji na Kata zianze kuwatumia askari wa mgambo ambao tayari wamepatiwa mafunzo wasaidie kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo hayo kwa kuwa idadi ya askari polisi bado ni ndogo “ aliagiza DC .
Baadhi ya madiwani walieleza kuwa katika kijiji cha Kasu kilichpo wilayani humo kuna kikundi cha kihalifu kinachojulikana Fwaku Fwaku ambapo juzi mama mmoja alibakwa lakini kwa aibu aliamua kunyamaza .
Mwisho
No comments:
Post a Comment