Sumbawanga
WAKAZI mkoani Rukwa wameshauriwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo unaodhaniwa kuwepo katika mkoa huo.
Kaimu mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Emmanuel Mtika alitoa tahadhari hiyo alipokuwa akizungumza na gazeti hili lilipotaka kujua kuhusiana na kuendelea kwa tishio la homa ya uti wa mgongo katika mkoa huo.
Alisema kuwa mpaka hivi sasa bado haijathibitika rasmi kama kuna homa ya uti wa mgongo ambayo inaambukizwa kwa njia ya hewa ambayo ndiyo huwa mbaya zaidi kwani vipimo bado havija thibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo.
Alisema kuwa awali kuna wagonjwa watano walipatikana mkoani humo wenyewe dalili za homa ya uti wa mgongo nani mgonjwa mmoja ambaye alifariki dunia siku chache zilizopita ambapo vipimo vya awali vilionesha kuwa alikuwa na vijidudu vya ugonjwa huo lakini kabla hawajafanya vipimo kwa awamu ya pili mgonjwa huyo alifariki dunia hali ambayo inashindwa kuthibitisha moja kwa moja kuwa kuna homa ya uti wa mgongo katika mkoa huo.
Mtika alisema kuwa wagonjwa wengine ambao walionesha dalili kama za kuugua ugonjwa huo walianzishiwa matibabu kwa nia ya kuokoa maisha yao kitendo ambacho kinaweza kusababisha majibu yasiwe ya uhakika kuwa ni homa hiyo ya uti wa mgongo kwakua tayari walianzishiwa matibabu kwa kutumia dalili ili kuokoa maisha ya wagonjwa hao.
Alisema kuwa kwa kawaida kuna aina nyingi za homa ya uti wa mgongo lakini iliyo hatari zaidi ni ile inayoambukizwa kwa njia ya hewa kwani zisipofanyika jitihada za dhati za kupambana nayo kunauwezekano watu wengi zaidi wakaugua na hali ikawa mbaya zaidi na kupoteza watu wengi kwa ugonjwa huo.
Dkt Mtika alisema kuwa mpaka kujiridhisha na kutangaza pasipo kuwa na shaka kuwa tayari kunaugonjwa huo ni lazima vipimo vifanyike zaidi ya Mara moja hivyo ni vizuri wananchi wa mkoa huo wakachukua tahadhari kwani wakifuata kanuni za kujikinga na ugonjwa huo pamoja na mengine, sambamba na matibabu yake kuna uwezekano mkubwa wa kudhibiti magonjwa mengi na kupunguza vifo.
Alisema wao kama sekta ya afya mkoani humo wana dhamana kubwa ya kuokoa maisha ya watu hivyo wanafanya kila liwezekanalo kwani hawafurahishwi na vifo vinavyotokea kwakua maisha yanamwisho basi na vifo vitokee kwa misingi ya kuwa mwisho umefika lakini kama kunauwezekano wa kukabili hilo ndilo jukumu lao la msingi.
Alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kuzingatia kanuni zote ambazo wamekuwa wakifundisha za kukabiliana na ugonjwa huo pamoja na mengine ili wananchi waishi maisha marefu waitumikie nchi pamoja na vizazi vyao vinavyo wategemea.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Hamidi Njovu aliwasihi wananchi wa halmashauri hiyo kuhakikisha wa naishi kwenye nyumba zenye hewa ya kutosha na kujiepusha kukaa kwenye mkusanyiko wa watu wengi kama hakuna umuhimu wa kufanya hivyo ili kuepuka ugonjwa huo.
Alisema kuwa mpaka hivi sasa bado halmashauri hiyo haijapiga marufuku mikusanyiko ya watu kama kwenye kumbi za sherehe, nyumba za ibada ama shughuli za mazishi ila alitoa tahadhari kwa wakazi wa Manispaa hiyo kujiepusha kwani kwenye mikusanyiko ya watu ndipo homa hiyo inaenea kwa Kasi kubwa kwakua inaambukizwa kwa njia ya hewa.
Aliwataka wananchi kutopuuzia kwenda kupata matibabu pindi wanapo jihisi kuugua na kuwa na utamaduni ya kupima magonjwa mbalimbali kwani kwa njia hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kukabiliana na magonjwa mengi kabla hayajafikia hali mbaya na kuchukua maisha ya wakazi wa Manispaa hiyo ambayo ndiyo nguvu ya uchumi katika Manispaa yake.
Mwisho
No comments:
Post a Comment