Sumbawanga
Kaimu
afisa mifugo wa Manispaa hiyo Abdala Abdala alizitaja kata ambazo
tayari zimeonekana nguruwe wake kuanza kuathirika na ugonjwa huo kuwa
ni kata ya Kizwite,kata ya lwiche, kata ya Katandala ambapo tayari
nguruwe wameonekana kuugua ugonjwa huo wa mafua ya nguruwe.
Akizungumza
na rukwakwanza.blogspot.com kaimu Afisa mifugo huyo alisema kuwa tayari imeanzishwa
karantini katika Manispaa ya sumbawanga ili kuzuia kuendelea kuenea kwa
ugonjwa huo ambao unawadhuru wanyama hao na si banaadamu hivyo ni
vizuri kukabiliana nao ili wanyama hao wasije wakafa na wakaisha kwa
ugonjwa huo.
Alisema
kuwa hapo awali ugonjwa huo uliripotiwa katika halmashauri nyingine za
mkoa huo lakini tayari umefika katika manispaa ya Sumbawanga na hii
imetokana na vimelea vya ugonjwa huo kuhamishwa kutoka huko ama na
nguruwe kutokana na biashara ya wanyama hao au binadamu ambao wanawagusa
na kula nyama yake hadi kufika katika Manispaa ya Sumbawanga.
Alizitaja
dalili za nguruwe wanapokuwa wamepatwa na mgonjwa wa mafua ya nguruwe
kuwa ni nguruwe hao kupata na homa kali na kuwa na rangi nyekundu
kuliko kawaida, manyoya yake kusimama na iwapo wafugaji wa nguruwe
wakiziona dalili hizo wanashauriwa kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya
ya mifugo wao watajua la kufanya.
Mmoja
wa wafugaji wa nguruwe katika Mji wa Sumbawanga Madanga Kayanza,
alisema kuwa awali alikua na hofu na usalama wake na familia kwa ujumla
lakini hofu ilipungua baada ya kuelezwa na wataalamu kuwa viini vya
mgonjwa huo havina madhara kwa binadamu ila kwa nguruwe lakini aliumia
tu iwapo nguruwe wake wataugua wanaweza kufa kwa mgonjwa huo.
Alisema
kuwa tatizo ni hasara ambayo unaweza kuipata kwakua yeye anafuga
nguruwe kwaajili ya kuuza na kujipatia kipato na ikitokea nguruwe wake
wakipata ugonjwa huo na kufa atakuwa amepata hasara kwakua akiwauza
ama kuwachinja na kuuza Nyama yake amekuwa akijipatia kipato kwaajili
ya kutatua changamoto nyingine katika maisha.
Mwisho
No comments:
Post a Comment