Wednesday, 2 August 2017

Madiwani Manispaa ya Sumbawanga wamchagua naibu Meya

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
BARAZA la madiwani la Sumbawanga mjini limefanya uchaguzi wa kumchagua naibu Meya pamoja na wenyeviti wa kamati mbalimbali za baraza hilo ambapo John Manyika ameibuka mshindi wa nafasi ya  naibu meya ambapo anatarajiwa kuliongoza baraza hilo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ijayo. 

Awali nafasi hiyo ilitangazwa kuwa inagombewa na wajumbe wawili ambao ni John Manyika kutoka CCM pamoja na Patrick Ngajiro kutoka Chadema,lakini Ngajiro alijitoa kugombea nafasi hiyo muda mfupi kabla ya uchaguzi.
Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Justine Malisawa akiongoza baraza la Madiwani. 


Akitangaza matokeo hayo katibu wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Hamidu Njovu alisema  kuwa siku ya uchaguzi wajumbe  wote 30 wa baraza hilo walihudhuria lakini waliopiga kura kumchagua naibu Meya walikua wajumbe 18 na alipata kura 16.
Wajumbe wa baraza hilo wanatokana na vyama viwili vya siasa ambavyo ni Chadema na CCM ambapo baadhi ya  wajumbe kutoka Chadema waliusia uchaguzi huo na kutoka nje baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu na kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo.
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

Katika uchaguzi huo pia walichaguliwa wenyeviti wa kamati mbalimbali zilizopo katika halmashauri hiyo, ambapo kamati ya mipango miji alichaguliwa Danieli Thomaas, kamati ya Afya elimu na uchumi alichaguliwa Norbeth Yamsebo, kamati ya Ukimwi John Manyika pamoja na kamati ya fedha alichaguliwa Justine Malisawa.
Mwisho

No comments:

Post a Comment