Monday, 5 June 2017

Sumbawanga vijijini kuadhimisha siku ya mazingira leo

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga

HALMASHAURI ya wilaya ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Leo inaadhimisha sherehe za Mazingira katika kijiji cha Milepa kilichopo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.

Sherehe hizo zitafanyika katika kijiji hicho lengo ni kuwahimiza wananchi katika kupanda miti katika bonde  hilo ambalo  ni tegemeo  kwa kilimo cha mpunga na Mahindi katika mkoa  wa Rukwa.

Akizungumza na rukwakwanza.blogspot.com Afisa habari wa halmashauri hiyo Ambwene  Yonah  Mwaifuge alisema kuwa taratibu zote zimekwisha andaliwa na maadhimisho yataanza majira ya saa  4 za asubuhi.

Katika sherehe hizo kutakua  na burudani mbalimbali ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Kalolo Ntila ambapo atatoa ujumbe mahususi katika suala zima  la  upandaji miti na uhifadhi wa mazingira.

Mwaifuge alisema kuwa jamii haina budi kutunza Mazingira ili iweze kutunza pia viumbe hai  wengine sambamba na kupata mvua zinazoanza kupungua kutokana na uharibifu wa Mazingira.

Aidha amewataka wakati wa bonde  hilo kujitokeza na kuhudhuria katika sherehe hizo kwani ni muhimu kwakua watapata elimu kuhusiana na utunzaji wa Mazingira.

Mwisho

No comments:

Post a Comment