Na Walter Mguluchuma
Katavi
TAFITI
zinaonesha kuwa mkoa wa Katavi katika kipindi cha mwaka 2015/ 2016
unamaambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa kiwango cha asimlia 14 na
Kitaifa maambuzi ya ugonjwa huo ni asilimia 14.8.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali mstaafu Raphael Muhuga wakati alipokuwa akifungua mkutano wa mpango wa ugawaji wa vyandarua kupitia katika vituo vya kutolea huduma za Afya na katika shule za Msingi uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda uliowashirikisha wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Katavi, Wakurugenzi wa Halmashauri Waganga wakuu wa Halmashauri na Maofisa Elimu.
Alisema tafiti za mwaka 2015/ 2016 zinaonyesha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria ni asilimia 114.8 Kitaifa na Mkoa wa Katavi ni asiliimia 14 wakati kwa mwaka 2008 maambukizi yalikuwa ni asilimia 9.1 Kitaifa na katika Mkoa wa Katavi ilikuwa ni asilimia 11.
Tangu wakati huo mpaka sasa kunaongezeko la asilimia tatu hivyo juhudi za makusudi bado zinahitajika ili kuweza kupunguza zaidi ya hapo kasi ya kuongezeka kwa ugonjwa huo .
Muhuga alisema kuwa Serikali kupitia wadau imeanzisha mpango
wa ugawaji wa vyandarua kwa jamii kupitia vituo vya
kutolea huduma ya afya kwa wajawazito na watoto chini ya umri wa
mwaka mmoja na wanafunzi katika shule za Msingi mkoani humo.
Afisa mipango wa Taifa wa kudhibiti malaria Oguda Josh alisema kwa kutumia mikakati mbalimbali, Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto ilidhamilia kuwa ifikapo mwaka 2016 maambukizi yawe yamepungua hadi asilimia tano na ifikapo mwaka 2020 maambukizi ya malaria yawe ni asilimia moja tu.
Alifafanua kuwa moja wapo ya mkakati wa kupunguza malaria ni ugawaji wa vyandarua kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya na shule za msingi.
Lengo la mkakati huo ni kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano hivyo utumiaji wa vyandarua uliosahihi utaweza kupunguza vifo kwa kiwango kikubwa.
Mratibu
wa Malaria wa Mkoa wa Katavi Dkt Benald Mbushi alieleza kuwa
Mkoa wa Katavi kumekuwepo kwa ongezeko la ugonjwa huo
kutokana na sababu mbalimbali.
Alizitaja baadhi
ya changamoto hizo kuwa ni kutofanyika kwa muda mrefu kampeni
za kuwahamasisha watu kudhibiti ugonjwa wa malaria kwenye maeneo yao ya kuishi na kwenye maeneo yao wanayofanyia kazi.
Pia
alisema changamoto ya miundo mbinu inayosababishwa na watu
wanaochimba mashimo ya kuchimbia madini na
wanao tengeneza barabara ambao wamekuwa wakichimba mashimo na
kuyaacha wazi bila kuyafukia na matokeo yake mashimo hayo yamekuwa ni
sehemu ya mazalia ya mbu .
Dr Mbushi alitaja changamoto
nyingine kuwa mbu siku hizi wamebadili tabia wamekuwa wakishinda
ndani ya nyumba wanazoishi watu na kumpumzika nje ya nyumba
hali inayosababisha kuwauma watu hata nyakati za mchana kirahisi.
mwisho
No comments:
Post a Comment