Wednesday, 9 August 2017

Rukwa yafanikiwa kupunguza Maleria

Na GurianAdolf
Sumbawanga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen ametoa wito kwa watekelezaji wa mpango wa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria katika Mkoa huo kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuepuka matatizo yaliyojitokeza katika mfumo uliotangulia.
Ametoa wito huo alipokuwa akifungua mkutano wa uhamasishaji kuhusu mpango wa ugawaji wa vyandarua kupitia vituo vya kutolea huduma za afya uliowashirikisha wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri na Mkoa.
Ugawaji huo wa vyandarua ulikuwa ukijulikana kwa jina la Hati Punguzo uliokuwa ukitumia vocha maaluma na kulipia Shilingi 500, mpango ambao ulisitishwa mwaka 2014 kutokana na ubadhirifu uliotokea kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ambapo watoa huduma walikuwa wakishirikiana na wakala kuandika vocha hewa na matokeo y a le wakala kuchukua fedha za umma bila kutoa huduma.
“kutokana na umuhimu wa kuwakinga wajawazito na watoto chini yamwaka mmoja Serikali imeamua kuanzisha tena utaratibu wa ugawaji wa vyandarua kwa mjamzito na mtoto chini yamwaka mmoja, moja kwa moja kutoka kwa mtoa huduma ya afya bila ya malipo yoyote wala uwakala,”  alisema Zelote.
Aliongeza kuwa lengo la mpango huo ni kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na ugonjwa wa malaria,pia kuongeza upatikanaji na utumiaji wa vyandarua katika ngazi ya kaya na jamii kwa asilimia 85 au zaidi na mwishoni mwa mwezi wa nane mwaka huu vyandarua hivyo vitaanza kugaiwa kwa mkoa wa Rukwa.
Kwa upande wake muuguzi mkuu mwandamizi kutoka wizara ya afya Epiphania Malingumu alisema kuwa mgawo wa vyandarua hivyo utafanyika kupitia bohari ya dawa (MSD) na vituo vya serikali pekee ndivyo vitaweza kutoa vyandarua hivyo kwakuwa vina namba maalum kwaajili ya malipo, hivyo vituo binafsi havitaweza kutoa huduma hiyo.
“Mama mjamzito atapata chandarua katika hudhurio la kwanza kliniki haitajalisha ni mimba ya miezi mingapi, kama amehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza akiwa na ujauzito wa miezi nane basi atapewa chandarua na mtoto akizaliwa atapewa tena chandarua na kama amejifungua mapacha basi atapewa vyandarua viwili,” Alisema Épiphania Malingumu.
Tafiti za mwaka 2015/2016 zinaonesha maambukizi ya ugonjwa wa malaria ni alimia 14.8 kitaifa na kwa Mkoa wa Rukwa ni asilimia 2.7. kwa mwaka 2012 maambukizi yalikuwa asilimia 9.5 kitaifa na kimkoa ilikuwa asilimia 4.5 ambayo imepungua kwa asilimia 1.8. 
Mwisho

No comments:

Post a Comment