Sumbawanga
Pombe hiyo
imechukua umaarufu mkubwa kutokana na kuuzwa kwa bei ya shilingi 1,200
ambapo ina ujazo wa mililita 200,na kiwango cha ulevi asilimi 42 ambayo
vijana wengi wakiwemo wanafunzi ndiyo wanatumia sana kilevi hicho.
Gazeti
hili likifanya mazungumzo na baadhi ya vijana wanaotumia kilevi hicho
walisema kuwa wameamua kuanza kutumia kwakua kinauzwa kwa bei naafuu na
kinapatikana katika maeneo mbalimbali ya kuuzia vilevi.
Mmoja
wa kijana huyo Francis Januari alisema kuwa kwasasa imekuwa ni ngumu
kupata viroba na badala yake wameamua kunywa pombe aina ya Win Vodka
ambayo imepata umaarufu kwakua bei yake ni chini ya kiroba ambapo
kabla ya kupigwa marufuku viroba vya konyagi vilikuwa vikiuzwa kwa bei
ya shilingi 1,500.
Mwandishi
wa gazeti hili alipita mtaani na kukuta kuna mwanafunzi mmoja
akilaumiwa na wenzake kuwa ameshindwa kuhudhuria shule baada ya kulewa
pombe aina ya Win Vodka na majirani wa mtoto huyo walisema kuwa
wanafunzi wengi wanakunywa pombe hiyo na kushindwa kuhudhuria vizuri
shuleni.
Hata hivyo
gazeti hili likiweza kuwasiliana na mganga Mkuu wa hospitali ya mkoa wa
Rukwa Emmanuel Mtika ambapo alisema kuwa pombe daima huwa siyo sawa kwa
matumizi ya afya ya binadamu bila kujali kiwango cha ulevi wala wapi
inatengenezwa.
Alisema
kuwa katika nchi yetu kuna tasisi kama TBS pamoja na TFDA ambazo ndizo
zinajukumu la kuhakiki ubora na usalama wa vyakula na dawa kwa
watumiaji wa hapa nchini na nivizuri kuhakikisha wanatumia bidhaa
ambazo zimethibitishwa na tasisi hizo.
Hata
hivyo baada ya kufanya uchunguzi katika kifungashio cha pombe hiyo ya
WIN VODKA ilibainika kuwa hakuna muhuri wa TBS wala TFDA ili
kuthibitisha kuwa wamekihakiki kilevi hicho na iwapo kinafaa kwa
matumizi hapa nchini.
Mwisho
No comments:
Post a Comment