Monday, 1 May 2017

Maporomoko ya mto Kalambo fursa ya kitalii mkoani Rukwa

Gurian Adolf
Sumbawanga

MOJA kati ya vivutio vya kitalii vilivyopo mkoani Rukwa ni maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls), maporomoko hayo yanapatikana katika wilaya ya Kalambo moja kati ya wilaya nne za mkoa wa Rukwa.

Yanaitwa maporomoko ya Kalambo kwasababu yapo katika mto Kalambo ambao upo mpakani kabisa mwa nchi ya Tanzania na Zambia.


             Maporomoko ya Mto Kalambo yaliyopo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.

Maporomoko hayo yapo nchini Tanzania lakini pia ukiwa ng’ambo ya nchi kwamaana kuwa ukiwa katika nchi ya Zambia unaweza kuyaona kwakuwa yapo mpakani kabisa ama bonde la maporomoko hayo ndilo linalotenga nisha nchi hizi yaani Tanzania na Zambia.

Maji yamto Kalambo ambao upo mkoani Rukwa katika wilaya ya Kalambo baada ya kuporomoka yanaingia katika ziwa Tanganyika.

Kijiji cha Kapozwa ambacho ndiyo kijiji kilichopo eneo ambalo yapo maporomoko ya Kalambo kinapatikana katika wilaya ya Kalambo katika mkoa wa Rukwa.

Maporomoko yamto Kalambo ni makubwa yanashika nafasi ya pili kwa ukubwa na marefu barani Afrika hivyo kuingia kwenye kumbukumbu za maporomoko makubwa katika bara hili.

Pamoja na kuwepo kwa maporomoko hayo lakini bado hayajatangazwa vya kutosha ambapo si ajabu wapo baadhi ya wakazi wa mkoa wa Rukwa hawajui chochote kuhusu Maporomoko hayo.

Ipo mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali hivi sasa katika kuhakikisha inaboresha mazingira napengine kuyatangaza maporomoko hayo ili yaweze kuvutia watalii ambapo kwa kutembelea tu ni wazi kuwa nchi yetu itapata fedha nyingi kutokana na tozo zitakazo tozwa kwa wageni na kiasi kidogo kwa wenyeji watakao hitaji kwenda kuyatembelea.

Ni vizuri sasa wananchi wakapata fursa ya kwenda kuyatembelea maporomoko hayo kwani hivi sasa serikali inajenga barabara kwa kiwango cha lami ambayo inaelekea katika bandari ya Kasanga ambapo ukifika katika kijiji cha Kawala unachepuka upande wa kushoto na kufuata katika barabara ambayo inaelekea katika kijiji cha Ngorotwa, Mpombwe na hatimaye Kapozwa ambako yapo maporomoko hayo.

Kwa maana hiyo unaweza kwenda katika Maporomoko ya mto Kalambo na kushuhudia na kurudi tena makao makuu ya wilaya ya Kalambo ama makao makuu ya Mkoa wa Rukwa ambao ni Manispaa ya Sumbawanga kwani ni umbali usiozidi kilomita 200 tu.

rukwakwanza.blogspot.com inatoa wito kwa watalii wa ndani na nje ya nchi kuyatembelea maporomoko hayo kwani watajionea uzuri wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu katika maporomoko hayo ambayo hayafanani na mengine yoyote kwa uzuri hapa duniani.

Nifursa sasa na ni wakati kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa na Katavi kubadirika ki fikra kwa kuamini kuwa kufanya utalii ni suala la wageni kutoka nje ya nje hususani wazungu.

Tasisi za kielimu pia zitumie fursa hiyo kufanya ziara ili walau wanafunzi wapate fursa ya kushuhudia maporomoko hayo kwani ni suala la aibu na ajabu kukuta Rogder Well mwanafunzi kutoka katika nchi ya marekani ambapo ni ma elfu ya kilometa akawa anayafahamu maporomoko hayo na kuyasimulia vizuri lakini si Katabi Sinyangwe mkazi wa Sumbawanga mjini ambapo haifiki hata umbali wa kilomita 200 eti hajui lolote kuhusu maporomoko hayo.

Mamlaka za serikali zitumie fursa mbalimbali kuendelea kuwasisitiza wananchi wa mikoa hii miwili na mingine kama inavyo fanya katika mataifa ya nje waweze kuyatembelea maporomoko hayo kwani kwa wananchi wa Tanzania ambao Mungu kawakirimia rasilimali hii tozo ni dogo kuliko wageni.

Wananchi wanapaswa kuyatembelea pamoja na kulipia fedha kwaajili ya kuushuhudia uzuri huo lakini pia wanaichangia fedha serikali yao ambazo bado zinarudi kuwahudumia wao wenyewe kutokana na mahitaji na matumizi ya serikali kupitia makusanyo na kisa bajeti ya nchi.

Tunawatakia kila lakheri katika kubadirika ki fikra na kuanza kuyatembelea maporomoko hayo ambayo hayapatikani sehemu nyinyine yoyote duniani.

   Mungu ibariki Tanzania, Mungu ubariki mkoa wa Rukwa,Mungu ibariki wilaya ya Kalambo!



No comments:

Post a Comment