Peti Siyame
Sumbawanga
MADIWANI
wa Halmshauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wamemjia
juu Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo , Simon Ngagani
wakimshinikiza asitishe mara moja mkataba alioingia na Wakala , Amri
Said
Nyambele kukusanya ushuru wa
mahindi kwamba ni batili.
Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo , Daudi Sichone ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo aliwahimiza madiwani hao waeleze kuwa wako tayari
halmashauri hiyo kuuvunja mkataba huo kwamba
iko pia tayari kulipa wakala
fidia ya mkataba ambao ni kiasi cha Sh milioni 16.
Hayo yalijiri katika kikao cha baraza la madiwani kilichoketi mwishoni mwa wiki katika Mji wa Matai ambapo kila upande
ulitupiana lawama ambapo Mkurugenzi Mtendaji , Ngagani alidai madiwani
hao wanaupiga vita mkataba
huo kwa maslahi yao binafsi huku
madiwani kwa upande wao
wakimlalamikia Ngagani kuwa ana maslahi na mkataba huo .
Pamoja
na vutanikuvute hiyo Ngagani alieleza kuwa hayupo tayari kuuvunja
mkataba huo kwa kuwa ulifuata taratibu zote za manunuzi isitoshe
ukivunjwa madhara yake ni makubwa kwa halmashauri hiyo.
“Mkataba huu unawalakini
una mapungufu makubwa nasema
hatuutambui usitishe mara moja hauna
maslahi kwa halmashauri yetu “ alieleza diwani Legius Boimanda.
Nae
diwani, Bernad Maskini alisisitiza kuwa mkataba huo ni batili
haukufuata utaratibu wa kufikishwa
mbele ya baraza la madiwani ili
waamue nani apewe uwakala wa kukusanya ushuru wa mahindi huku
akisisitza kuwa wakala Nyambele ana sifa hiyo kwa kuwa nae ni
mfanyabiashara
wa nafaka .
Diwani , Peter
Simuyemba alishauri halmashauri iingie
mkataba na Serikali ya Vijiji ya
ukusanyaqji wa ushuru wa mahindi ambapo watapanga malengo ya makusanyo
hayo badala ya kuendelea kuwakumbatia mawakala ambao wengi wao sio waaminifu .
“Vitu viwe wazi ...
msitupige pige chenga mkataba huu haukupitishwa na sisi madiwani
uvunjwe mara moja kwani
hatuutambui “Diwani Edwin Msipi
Nae Mwenyekiti wa baraza hilo Sichone alilazimika mara
kwa mara akiwataka madiwani
waeleze wazi kuwa wako tayari mktaba huo uvunjwe na fidia
ya mkataba kuilipwe kuliko kuendelea nao .
Mkurugenzi Mtendaji Ngagani akifafanua aliwaeleza madiwani hao
kuwa Kamati ya Fedha na Mipango imekasimiwa madaraka
ya kuteua wakala ambapo
Mkurugenzi Mtendaji akisaini unakuwa
ni mkataba halali ambapo utaletwa
mbele ya baraza la madiwani kama taarifa na si vinginevyo .
“Sababu
za kuuvunja mktaba huu sijaziona ..ubadhilifu haupo kwa kuwa wakala
atakusanya ushuru kwa
kutumia mashine za kielektroniki …taratibu zote za manunuzi zilifuatwa
sijaelewa kwanini hamu mtaki wakala huyu sasa mnataka niamini
niliyoyasikia kuwa baadhi yenu
mnawataka maofisa watendaji wa vijiji ili iwe rahisi kupiga nao
dili''.. alisema
Kwani hamtaki huyu wakala
wa mazao wakati ambapo tuna
mawakala wengine mnadani
kwanini nao hamjawakataa? Lazima
kuna jambo sio bure” alisisitiza .
Akifafanua alisema kuwa wakala Nyambele kwa kipindi cha mwezi mmoja tu ameweza kukusanya
zaidi ya Sh milioni 26 ikiwa ni ushuru wa mahindi tu kwamba
mktaba wake ni wa miezi
mitatu ambapo sasa imebaki miezi miwili ambapo ukivunjwa mktaba
halmshauri italazimika kumlipa fidia
ya mktaba ambayo ni aslimia 20 ya
makusanyo hivyo italazimika kumlipa kiasi cha Sh milioni 16 .
“Katika kikao cha Kamati ya Fedha na Mipango wajumbe nane
walimkubali wakala huyo huku mmoja
akipinga …tutaongea sana kuuvunja
mktaba huu sio rahisi isitoshe hadi sasa sijaona sababu za maana kinachoshangaza hata madiwani wa CCM
waliukataa hata kwenye vizuizi vya mazao
asiwekwe mtu inanitia shaka
sana lakini kwanini hamuwazungumzii
wakala wa minadani''
Mnataka halmashauri iwarudishe
maofisa watendaj wa vijiji
wakusanye ushuru wa mazao ili
madiwani wanufaike kwakuwa walishazoea wanapatapata kitu kidogo iwapo
kama mtavunja mkataba huu
niwakikishie halmshauri hii itayumba kifedha na itakuwa hatarini
kuvunjika “ alisisitiza .
Alifafanua kuwa Kamati ya Fedha na Mipango ikiridhia
na Mkurugenzi Mtendaji akitia saini tayari ni mkataba halali .
Kaimu Mwanasheria wa
Halmshauri hiyo , Tutalemwa Mwenda aliwatahadharisha
madiwani hao kuwa iwapo kama mkataba
huo utavunjwa basi wakala
atalipwa fidia ya mktaba ambayo ni Sh milioni 16 za bure kwa miezi miwili ambayo hajafanyika
kazi .
Ndipo Mwenyekiti Sichone alipoomba
ushauri kutoka kwa washiriki baada ya kupata ufafanuzi wa kisheria kutoka
kwa Kaimu Mwanasheria Mwenda.
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kalambo , Hilaly Kazumba
alishauri ili halmashaurihiyo isipate
hasara imwache wakala huyo amalize miezi miwili iiyobakia .
Nae Katibu wa CCM wa wilaya ya Kalambo , Robert Mwiga aliwataka
madiwani hao wasitoe maamuzi ambayo
yataitia hasara halmshauri yao .
Akichangia Katibu Tawala wa Wilaya ya Kalambo , Frank Sichalwe alisema madiwani wakiendelea kushikilia
msimamo wao huo wataiingiza halmashauri hiyo katika mgogoro mkubwa.
Baada
ya kutolewa kwa ushauri huo ndipo Diwani Peter Simuyemba alipotaka
madiwani wapige kura ili kuumaliza mzozo huo ambao kura 15 hazikutaka
mkataba huo
uvunjwe huku tano zikitaka uvunjwe
.
Gazeti hili lilizungumza
na baadhi ya madiwani na waalikwa kando ya kikao hicho kwa masharti
ya kutoandikwa majina yao gezetini ambapo madiwani walikiri kuwa
waliketi kikao cha siri na kukubaliana mkataba huo uvunjwe .
“Nashangaa sana
mwishoni tumegawanyika tuliketi
na kukubaliana kwa pamoja mkataba
huu ni batili uvunjwe lakini tumeshindwa
tulikubaliana kuwa
hata kama wakala huyu afanye vizuri au la hatumtaki “ alisema
mmoja wao .
Baadhi ya waalikwa walidai kuwa madiwani hawamtaki wakala huyo kwa kuwa atawabana kwa kuwa wengi wao ni wakulima wakubwa wa
mahindi kwamba wanataka wakala ambaye
watamteua wao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment