Gurian Adolf
Sumbawanga
Baadhi
ya wanachama wa chama cha mapinduzi(CCM) ambao nafasi zao zimefutwa
kutokana na maboresha yaliyofanyika na mkutano mkuu hivi karibuni
wametakiwa kuacha kujiona wanyonge kwakua bado ni wanachama kamili na
wanahadhi sawa na wanachama wengine.
Wito
huo umetolewa jana na mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya jumuia ya
wazazi CCM mkoa wa Rukwa Ponsian Nyami wakati akiwasalimia wajumbe wa
kikao maalumu cha kuzindua kamati ya kuchangia fedha kwaajili ya
uchaguzi wa jumuia hiyo mkoani humo.
Alisema
kuwa wapo baadhi ya wajumbe katika ngazi mbalimbali ambao nafasi
walizokuwa nazo zilifutwa kufuatia maboresho ya chama hicho kuacha
kujiona wanyonge na kuamini kuwa wao ni wana CCM wa zamani.
Nyami
alisema kuwa kutokana na nafasi hizo kufutwa waliobakia wanaitwa wana
CCM wa Magufuli hivyo kusababisha kuibuka kwa makundi mawili ambayo ni
wana CCM wa mwenyekiti Magufuli na wanachama wa zamani.
Alisema
kuwa wanachama wote ni wa CCM isipokuwa ni maboresho ambayo yamefanyika
kutokana na wakati hivyo hakuna aliyebora zaidi ya mwingine ndani ya
chama hicho.
Kwaupande
wake mwenyekiti wa jumuia ya wazazi ya CCM mkoa wa Rukwa Rainer Lukara
alisema kuwa wanachama watakao jitokeza kugombea nafasi mbalimbali
katika jumuia hiyo wanapaswa kutambua kuwa rushwa ni adui wa haki na
kamwe atakae toa rushwa hata vumiliwa.
Alisema
kuwa jumuia ya wazazi ndiyo inajukumu la kukilea chama na jumuia zake
hivyo ni vizuri uchaguzi wa jumuia wao uwe ni wa mfano kwani itakuwa ni
fedheha iwapo uchaguzi wa jumuia hiyo utagubikwa na rushwa.
Lukara
aliwasisitiza wajumbe wa jumuia hiyo kuhakikisha kuwa wanaongeza
wanachama wa jumuia hiyo na chama kwa ujumla kwani hivi sasa watu
waliowengi wanavutiwa na utendaji kazi wa mwenyekiti huyo hivyo watumie
fursa hiyo kuongeza wanachama wa CCM pamoja na kuwarudisha wale
waliokihama chama kabla ya uchaguzi mkuu uliopita.
Alitoa
wito kwa wajumbe wa kamati ya uchangishaji fedha kwaajili ya uchaguzi
kujituma kufanya hivyo kwa kupitia kwa wanachama na wadau mbalimbali ili
suala la mgombea kufadhili uchaguzi peke yake na matokeo yake wajumbe
kujiona ni lazima wamchague kwakuwa amefadhili mchakato mzima wa
uchaguzi ndani ya chama na katika jumuia zake.
Mwisho
No comments:
Post a Comment