Walter Mguluchuma
Katavi
WALIMU wa shule ya Msingi
Mtapemba katika Halmashauri ya Nsimbo Wilaya
ya Mpanda Mkoani Katavi wanalazimika kukesha pindi mvua
zinapoanza kunyesha nyakati za usiku kutokana na kuvuja na hofu ya kubomokewa
na nyumba za shule ambazo zimechakaa kiasi cha kutofaa kuishi binadamu.
Nyumba ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo pia
haina hata choo hali inayomsababishia usumbufu yeye na familia yake wakati
wa usiku pindi wanapotaka kujisaidia kwani wakati wa mchana wamekuwa akienda
kuomba kujisaidia katika vyoo vya majirani zake.
Shule hiyo ya
Msingi ambayo ilijengwa zaidi ya 40 iliyopita ipo
umbali wa kilometa kumi na tano kutoka Manispaa ya Mji
wa Mpanda inajumla ya walimu 16.
Mfano wa nyumba mbovu zilizojengwa kwa tope
Walimu wa shule hiyo
wanalazimika kuishi kwenye nyumba za kupanga kijijini
hapo na wengine kuishi katika kijiji cha jirani
kutokana na shule hiyo kuwa na uhaba wa nyumba
za walimu.
Nyumba ambayo imejengwa kwa
ajiri ya kuishi mwalimu Mkuu wa shule
hiyo haina choo hali ambayo inafanya
mwalimu anae ishi kwenye nyumba hiyo kutumia vyoo
vya kuomba kwa jirani zake hali ambayo inamvunjia heshima na inamfanya ajisikie
aibu kuomba kujisaidia kwa majirani yeye pamoja na familia yake.
Baadhi ya nyumba
zilizopo katika shule hiyo ni chakavu
sana na hazifai kuishi na zimejengwa kwa tofali udogo
sio tofali za kuchoma na hivyo si nyumba imara na zinaweza kubomoka
wakati wowote.
Mmoja wa walimu anae
ishi kwenye nyumba hizo ambae hakutaka kutaja
jina lake alisema huwa wanalazimika kutolala usiku pindi mvua
zinapokuwa zinanyesha kutoka na nyumba wanazoishi kuvuja na hofu ya
kuangukiwa na nyumba hizo ambazo si imara kutokana na kujengwa kwa matofali ya
tope.
Kwa upande wake Diwani wa Kata
hiyo ya Mtapemba Elieza Fyula alikiri kuwaepo kwa tatizo la
uhaba wa nyumba katika shule hiyo kwa kipindi
kirefu sasa na alisema kuwa hakuna mpango wowote wa kujenga nyumba katika
shule hiyo.
Alisema shule hiyo licha
ya kuwa na walimu 16 inazo nyumba tano kati ya hizo moja
ndio imejengwa kwa tofali za kuchoma kwa nguvu ya wananchi na
nyumba nyingine zimejengwa kwa tofali za tope na ziko katika hli
mbaya ya uchakavu.
Alifafanua kuwa
changamoto ya nyumba za kuishi walimu katika shule
hiyo imesababishwa na Halmashauri ya Nsimbo kutotenga fedha kwa ajili
ya ujenzi wa nyumba za walimu licha ya yeye diwani kuishauri
Halmashauri lakini imekuwa haitengi fedha kwaajili ya
kuboresha mazingira ya watumishi hao wa idara ya elimu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment