Friday, 21 April 2017

Tasisi ya MIICO yawajengea uwezo wakulima wilayani Sumbawanga wafanye kilimo mseto

  
Gurian Adolf
Sumbawanga

WAKULIMA wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wameshauriwa kulima kilimo mseto ambacho kinahusisha upandaji wa miti ya aina tofauti ndani ya mashamba yao ambayo itawapa tija kutokana na kilimo pamoja na mazao yatokanayo na miti itakakayopandwa shamaba yao.

(picha ni baadhi ya wakulima kutoka katika kata tatu za Msanda Muungano,Msandulula na Mpwapwa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wakijengewa uwezo ili waweze kulima kilimo mseto.)

Akichangia mada katika mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na taasisi ya kuwajengea uwezo katika kilimo mseto ya MIICO, afisa kikimo wa wilaya ya Sumbawanga Habona Kwileluye alisema kuwa kilimo hicho kinatija kubwa kwakuwa miti watakayopanda katika mashamba yao watanufaika sana.

Alisema kuwa iwapo mkulima atalima mazao ya chakula sambamba nakupanda  baadhi ya miti kama ya matunda ambayo pia watapata mazao kutokana na miti ambayo watapanda katika mashamba yao. 

                         
Alisema kuwa iwapo mkulima atalima mahindi na ndani ya shamba lake akipanda miti ya matunda kama ya miparachichi na miti ya aina nyingine, mkulima atanufaika kwa kuvuna mazao na kisha miti ikikuwa ataendelea kunufaika na matunda yatakayo tokana na miti hiyo ikiwemo ni pamoja na mbao.

Alisema kuwa wakulima wasiwe na hofu katika kupokea kilimo kwani katika baadhi ya mikoa hapa nchini kimeonekana kuwanufaisha wananchi na kuweza kuondokana na umasikini.

 (picha Gloria Mdindile kutoka tasisi ya MIICO akiwasilisha mada kuhusiana na umuhimu wa kilimo  mseto.) 

Akizungumza katika mafunzo hayo kwa niaba ya mkurugenzi makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Rashid Kalele alisema kuwa maofisa ugani wanapaswa kushirikiana na wakulima kwa kuwapa elimi ili mradi huo uweze kufanikiwa.

Awali akiwasilisha mada katika mafunzo hayo Gloria Mdindile kutoka tasisi ya MIICO alisema kuwa mradi huo utatekelezwa kwanza katika kata tatu za wilaya hiyo ambazo ni Msanda Muungano, Kata ya Msandulula na kata ya Mpwapwa zitakuwa ni za majaribio na iwapo ukifanikiwa utatekelezwa katika wilaya nzima.

Alisema kuwa mpaka hivi sasa tasisi hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 60 kwaajili ya kutoa mafunzo kwa wakulima ikiwa ni kuwajengea uwezo iwapo mradi huo utafanikiwa katika kata hizo wataongeza bajeti kwaajili ya kuutekeleza katika wilaya nzima.
Mwisho

No comments:

Post a Comment