Tuesday, 18 April 2017
Plan International yawakomboa wasichana 360 Nkasi
Gurian Adolf
Nkasi
WATOTO wa kike wapatao 360 kati ya umri wa miaka 12 hadi 24 kutoka katika vijiji 13 wilayani Nkasi mkoani Rukwa, ambao wamepitia changamoto kadhaa za kimaisha ikiwemo ni pamoja na kupata mimba na kuolewa katika umri mdogo wameanza kupata mafunzo ya ujuzi ili waweza kukabiliana na maisha baada ya ndoto zao za kuendelea na masomo kukwama.
Mafunzo hayo yanayotolewa na chuo cha Maendeleo Chala (FDC) yamefadhiliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la PlanInternational yamelenga kuwapatia ujuzi watoto hao ili waweze kujiajili kupitia taaluma watakazozipata na kuweza kuendesha maisha.
Mmoja wa Wakufunzi wa mafunzo ya ushonaji Grace Kifyoga amesema kuwa mafunzo watakayoyapata watoto hao kwa kipindi hiki cha miezi sita yatawawezesha kabisa kupata ujuzi wa kutosha na kuweza kuutumia ujuzi huo kuweza kujishughulisha na kupata kipato na kuweza kupata uwezo wa kuepuka vishawishi kutoka kwa Wanaume waliuopelekea hapo awali kushindwa kumaliza elimu zao baada ya kupata mimba au kuolewa katika umri mdogo.
Amedai kuwa kwa sasa wanafunzi hao wanapata ujuzi katika taaluma za ufundi wa umeme na ushonaji na kuwa toka waanze mafunzo hayo inaonyesha dalili njema kwa watoto hao ya kuweza kufanya vizuri katika mafunzo yao hayo.
Mratibu wa ndoa za utotoni kutoka Plan International Nestory Frank amesema kuwa taasisi yao imeonelea kutoa mafunzo hayo kama njia ya kudumu ya kuwaondolea changamoto za kimaisha watoto hao ambao ndoto zao zilikwamishwa na mimba na ndoa katika umri mdogo.
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment