Sumbawanga.
Msichana
huyo ambaye hakuweza kufahamika jina lake Mara moja jana alivuliwa
nguo na wapiga debe wa stendi kuu baada ya kufika katika stendi hiyo
ambayo haikufahamika Mara moja alikuwa amekwenda kufanya nini.
Picha ya Msichana akiwa amedharirishwa baada ya kuchaniwa nguo.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo Issa Daniel ambaye ni mfanyabiashara
ndogondogo ya kuuza urembo katika stendi hiyo alisema kuwa akiwa amekaa
katika kibanda chake ghafla alisikia kelele za watu na alipotoka nje
aliwaona wapiga debe hao wakiwa na watu wengine wakimfukuza msichana
huyo.
Baada ya kufanikiwa
kumkamata walimchania sketi aliyokuwa amevaa wakidai kuwa wamechishwa
na tabia ya wanawake ambao wake kuwa wakifika katika stendi hiyo huku
wakiwa wamevaa nguo fupi almaarufu kama mini sketi.
Baada
ya tukio hilo baadhi ya wanawake walikuwa pembeni wakishuhudia tukio
hilo walimchukua msichana huyo na kumwingiza kwenye chumba kimoja
ambacho kipo karibu na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambapo
walimpa kanga ili ajisetiri kufuatia tukio hilo.
Daniel
alisema kutokana na kitendo hicho baadhi ya watu walilaani kitendo
hicho na kuliomba jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine kuchukua
hatua kufuatia tukio hilo.
"Hata
kama alikuwa amevaa nguo fupi hawakupaswa kumfanyia vile kwani ule ni
udhalilishaji wa hali ya juu wangemwambia lakini si kumchania sketi
yake na kubaki na nguo ya ndani(chupi) kwakweli ni udhalilishaji wa
hali ya juu"... Alisema.
Alisema
baada ya tukio hilo aliwaona polisi wakiwa wamefika katika eneo la
stendi kuu ambapo walianza kuwasaka wahusika wa tukio hilo na aliomba
iwapo watakamatwa wachukuliwe hatua kwani kitendo kile kamwe hakiwezi
kuvumilika katika jamii ya watu wastarabu.
Aidha
kufuatia tukio hilo baadhi ya watu walipiga picha kwa kutumia simu zao
za mkononi na kuchukua video kisha kuweka katika mitandao ya kijamii
ikiwemo facebook na what's up ili watu waweze kuona kile kilichotokea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment