Tuesday, 25 April 2017

Rushwa ya fedha bado yalalamikiwa mkoani Katavi

Walter Nguluchuma
 Katavi 
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda  pamoja na  Halmashauri ya  Wilaya ya Mpanda  katika  Mkoa wa  Katavi  kwa  kipindi cha   kuanzia   Julai  2016  hadi  Machi 2017  zimeongoza kati  ya   Halmashauri zote zilizopo  katika  Mkoa huu  kwa   malamiko yanayo  husiana  na  Rushwa.

Hayo yalisemwa  jana  na  Kaimu wa TAKUKURU  Mkoa wa  Katavi   Cristophar Nakua  alipokuwa  akitoa  taarifa kwa wandishi wa  Habari  ofisini  kwake taarifa  ya  utekelezaji  wa  shughuli zao za  kipindi cha kuanzia  mwezi  Julai  2016  hadi  Machi  2017.

Alisema  katika  kutekeleza  majukumu yake TAKUKURU   Mkoa wa  Katavi  kwa  kipindi cha kuanzia  Julai  2016  hadi Machi 2017 imepokea  malalamiko ya vitendo vya  rushwa  83 na kufungua  majalada 28 ya  uchunguzi huku ofisi hiyo  ikiwa  na  jumla ya   majalada  ya uchunguzi  118  yanayoendelea na uchunguzi

Alieleza  kuwa wakati   huo huo  taarifa nyingine  zinaendelea  kufanyiwa kazi na zipo katika  hatua  mbalimbali  za chunguzi  zilizofanyika  na  zinazoendelea na TAKUKURU   Mkoa wa  Katavi  imefanikiwa  kuokoa   kiasi cha tsh 10,425,000.

 Alifafanua kuwa   taarifa  zilizopokelewa na  zimebainisha  Wizara  mbalimbali  zinazotuhumiwa  na vitendo vya Rushwa  kuwa ni taasisi za  Serikali  na  Sekta  binafsi  huku  Wizara  inayoongoza  kwa  malalamiko  mengi ni TAMISEMI   yenye  malalamiko 68, Wizara ya  Mambo ya  ndani  sita ,Wizara ya  Katiba na  Sheria  manne, Wizara ya Nishati na  Madini  mawili, Wizara ya  Fedha lalamiko moja na  Sekta  Binafsi   mawili.
Kaimu wa mkuu wa TAKUKURU  Mkoa wa  Katavi   Cristophar Nakua akitoa taarifa kwa wandishi wa habari(hawapo kwenye picha)

Kaimu  Mkuu huyo wa  TAKUKURU Mkoa wa  Katavi  alisema  katika  tathimini  iliyofanyika  katika  kipindi  hicho   inaonyesha kuwa   Halmashauri ya  Manispaa ya  Mpanda   na  Halmashauri ya  Wilaya ya Mpanda  ndio   zinaongoza   kwa kuwa na  malalamiko  25 kila  moja  ikifuatiwa  na  Halmashauri  ya  Wilaya ya  Nsimbo  yenye  malalamiko 11,  Halmashauri ya  Wilaya ya  Mlele  malalamiko manne na  Halmashauri ya  Mpimbwe  yenye  malalamiko  matatu.

Alisema TAKUKURU  wataendele kutoa  elimu   kwa  njia  mbalimbali ya kuielimisha jamii   juu ya  madhara ya tokanayo  na  rushwa.
mwisho

No comments:

Post a Comment