Gurian Adolf
Nkasi
DIWANI
wa kata ya Mkwamba wilayani Nkasi, Chiluba Mwandamo amewapiga marufuku
baadhi ya watendaji wa vijiji vilivyopo katika kata hiyo kuacha tabia ya
kuigeuza misiba inayotokea katika vijiji vyao na kuwa mikutano ya
vijiji.
Marufuku hiyo aliitoa jana katika kikao cha
maendeleo ya kata hiyo WODC alipokuwa akizungumzia suala la tabia ya
watendaji hao kutokuwa na utamaduni wa kuwasomea wananchi mapato na
matumizi ya vijiji.
Alisema kuwa wapo baadhi ya watendaji
ambao wamekuwa na tabia ya kusimama katika misiba iliyopo vijijini kwao
na kuanza kutoa maagizo ya serikali kwa kisingizio kuwa wananchi
hawahudhurii mikutano ya vijiji.
Diwani huyo alisema kuwa
kwakuwa eneo hilo linakuwa ni lamsiba baadhi yao wanatumia mwanya huo
kwakuwa wanajua watu watakua katika maombolezo na hivyo hawatakuwa na
uwezo wa kuuliza maswali.
Mwandamo alisema kuwa wapo baadhi
ya watendaji ambao wamekuwa wakidiriki hata kusoma mapato na matumizi
ya kijiji hali ambayo si sawa kwani eneo hilo ni la maombolezo na
wananchi wanakuwa na hudhuni kwa hiyo hawawezi kufuatilia taarifa za
mapato na matumizi kwa ufasaha.
Alitoa wito kwa wananchi
kuwafukuza katika eneo la msiba watendaji wenyetabia hiyo hiyo kwani
wananpaswa wawe wanaitisha mikutano yao kwaajili ya kuzungumza na
wananchi.
Mmoja wa wananchi wa kata hiyo Mariamu Kanana
alimshukuru diwani huyo kwa uamuzi huo kwani alisema kuwa wananchi
walikuwa wanakerwa na tabia hiyo lakini walikuwa wananshindwa kuwaambia.
Alisema
kuwa watendaji hao hawanabudi kuitisha mikutano yao ya vijiji kama
wananchi hawatakuwa wanahudhuria watafute njia ya kuwabana ili
wahudhurie lakini si kugeuza misiba katika kata hiyo kuwa mikutano ya
vijiji.
mwisho
No comments:
Post a Comment