Wednesday, 27 May 2015

Mamilioni hawana maji safi ya kunywa Yemen


Yemen
Takriban thuluthi mbili ya wakaazi wa Yemen hawana njia ya kupata maji safi ya kunywa, miezi miwili tangu nchi shirika zinazoongozwa na Saudi Arabia kuanza hujuma zao dhidi ya vikosi vya waasi. 
Habari hizo zimetangazwa na shirika la misaada la Oxfam.”Hujuma za angani, mapigano ya nchi kavu na upungufu wa mafuta yanawafanya Wayemen milioni tatu zaidi kukosa maji safi ya kunywa na kuifanya idadi ya Wayemen wanaoishi bila maji na vyoo kufikia watu milioni 16-shirika hilo lenye makao yake nchini Uengereza limesema. “Idadi hiyo ni sawa na wakaazi wa Berlin, London, Paris na Roma kwa pamoja” mkurugenzi wa tawi la Oxfam nchini Yemen, Grace Ommer amesema katika taarifa yake. Nchi shirika zinazoongozwa na Saudi Arabia zimeanza mashambulio ya angani tangu Machi 26 mwaka huu dhidi ya waasi wa Houthi na washirika wao – wanajeshi wamaomtii rais wa zamani wa Yemen Ali Abdallah Saleh – kwa lengo la kumrejesha madarakani rais anayeungwa mkono na Umoja wa mataifa Abedrabbo Mansur Hadi. “Watu wanalazimika kunywa maji machafu na kuzidisha hatari ya kushikwa na maradhi mfano wa Malaria, kipindupindu na tumbo la kuendesha -shirika hilo la Oxfam limeendelea kusema.

No comments:

Post a Comment